SITARAJII KUTENDEWA HAKI TFF:WAMBURA

MGOMBEA wa nafasi ya Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoani Mara (FAM), Michael Wambura amesema hatarajii kupata haki kutoka Kamati ya Rufaa kuhusu pingamizi lililowasilishwa dhidi yake kwa sababu mbalimbali alizoziona.

Akizungumza na waandishi wa Habari katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Wambura alisema inaonekana Shirikisho la soka Tanzania (TFF) lina mikakati ya kumuondoa kuwania nafasi aliyoiomba wakati si nafasi yao kufanya hivyo bali kazi hiyo inatakiwa ifanwe na Wadau wa soka mkoa wa Mara.
Wambura alisema anatarajia kuwasilisha baadhi ya taarifa za fedha za TFF kwa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa Tanzania (TAKUKURU) na taarifa za kuomba haki ya kisheria kwa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (Tanganyika Law Of Society) kufuatia kutotendewa haki katika mkutano wa juzi dhidi yake na Kamati ya rufaa.
Alisema taarifa za fedha kupitia stakabadhi zitakazowasilishwa TAKUKURU ni kuanzia Oktba 16 hadi 20 kwa mlolongo wa namba za risiti za michezo na rufaa iliyowasilishwa dhidi yake.
Alisema taarifa hizo ataziwasilishwa TAKUKURU kwa muonekano kuna mianya ya rushwa baina ya Shirikisho hilo.
Aidha Wambura alisema mbali ya taarifa hizo za rushwa pia atawasilisha taarifa za malalamiko ya kisheria dhidi ya viongozi wa Kamati ya rufaa akiwalalamikia wanasheria Hamidu Mbwezeleni na Karua wanaozuia kupata msaada wa kisheria na haki ya kutetewa na mawakili jambo ambalo kimtazamo ni kinyume na malengo na misingi ya chama hicho.
Alisema baada ya kupitia malalamiko aligundua kwamba Titus Osoro hakukata rufaa kama barua ya TFF ilivyonakiliwa wakati Kamati ya rufaa haisikilizi pingamizi ikiwa pia mlalamikaji hakuweka pingamizi katika kamati ya uchaguzi mkoa wa Mara.
Wambura alisema mlalamikaji aliwasilisha pingamizi bila kuambatanisha malipo ya shilingi 500,000 ikiwa barua ya mlalamikaji ilipokelewa Oktoba 18 na mmalipo ya stakabadhi ya TFF No 0164 ya Oktoba 20 na baadaye kufutwa na kuandikwa Oktoba 19.
Alisema risiti namba 0164 ya malipo ya rufaa ilifanyiwa marekebisho na kufutwa Oktoba 20 na nnasomeka Oktoba 19 ili ionekane rufaa ilikatwa na kupokelewa ndani ya siku ya rufaa wakati kikao cha kupitia mapingamizi cha FAM kiliketi Oktoba 15 ambako mwisho wa rufaa ulikuwa ni Oktoba 19 na rufaa hiyo ilikuwa nje ya muda.

Post a Comment

Previous Post Next Post