SUMA LEE ASHUKURU MASHABIKI KUIPOKEA 'HAKUNAGA'


MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ismail Sadiki ‘Suma Lee’, ameelezea kuridhishwa na mapokezi kutoka kwa wadau na mashabiki wa muziki nchini katika wimbo wake mpya ‘Hakunaga’ na akaomba sapoti hiyo iendelee hadi atakapoiingiza sokoni albamu yenye wimbo huo.
Suma Lee alisema kuwa furaha yake itakamilika iwapo wapenzi wa muziki nchini na wananchi kwa ujumla watamuunga mkono kwa kuinunua albamu yake mpya aliyoipa jina la ‘Hesabu za Mapenzi’, ambayo itaujumuisha wimbo huo wa ‘Hakunaga’ ambayo imebeba nyimbo 15.
Alisema kwamba kutokana na makubaliano yake na wasambazaji, albamu hiyo itaingia sokoni hivi karibuni, lakini ni wapenzi wa muziki na wananchi kwa ujumla watakaoamua thamani ya albamu hiyo kwa kuinunua.
“Nachukua fursa hii kuwashukuru wapenzi wa muziki na wananchi kwa ujumla kwa kuupa sapoti wimbo wangu wa ‘Hakunaga’ ambao ni moja ya nyimbo zinazoitangaza albamu yangu mpya ya ‘Hesabu za Mapenzi’, hata hivyo ninawaomba waniunge mkono zaidi kwa kuinunua albamu hii pale itakapoingia sokoni,” alisema.

Post a Comment

Previous Post Next Post