STARS YAPANGIWA MSUMBIJI CAN 2013

Tanzania (Taifa Stars) imepangwa kucheza na Msumbiji katika kinyang’anyiro cha kutafuta tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika mwaka 2013 nchini Afrika Kusini.
Upangaji ratiba wa mechi hizo za mchujo ulifanywa juzi (Oktoba 28 mwaka huu) na kamati ndogo ya michuano hiyo mjini Malabo, Equatorial Guinea
Jumla ya nchi 47 ikiwemo mwenyeji Afrika Kusini ndizo zilizothibitisha kucheza michuano hiyo. Nchi 16 zilizofuzu kucheza fainali za mwakani nchini Gabon na Equatorial Guinea zenyewe zimepitishwa moja kwa moja hadi raundi ya mwisho ya mchujo itakayoanza baada ya fainali za 2012.
Raundi ya kwanza ya awali itahusisha nchi nne ambazo kwenye ubora wa viwango ndizo ziko chini ili kupata mbili zitakazoingia raundi ya pili ya awali itakayokuwa na nchi 28. Nchi hizo ni Swaziland, Sao Tome, Lesotho na Shelisheli.
Stars imepangiwa kucheza na Msumbiji katika raundi hiyo ya pili ya awali. Tarehe za mechi hizo ambazo zitachezwa katika nusu ya kwanza ya mwaka 2012 zitatangazwa baadaye.
Mechi nyingine za raundi hiyo zitakuwa kati ya Ethiopia na Benin, Rwanda na Nigeria, Congo na Uganda, Burundi na Zimbabwe, Algeria na Gambia, Kenya na Togo, Sierra Leone na mshindi kati ya Sao Tome na Lesotho.
Nyingine ni Guinea Bissau na Cameroon, Chad na Malawi, mshindi kati ya Shelisheli na Swaziland dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Misri, Madagascar na Cape Verde na Liberia na Namibia.
Timu 14 zitakazopita hatua hiyo zitaungana na 16 zilizofuzu kwa ajili ya fainali za Gabon/Equatorial Guinea kucheza raundi ya mwisho kupata 15 zitakazoungana na wenyeji Afrika Kusini kwa ajili ya fainali za 2013. Raundi hiyo itachezwa kati ya Septemba na Oktoba mwakani.

LIGI KUU YA VODACOM
Mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom unamalizika wiki hii kwa mechi zifuatavyo;
Oktoba 30- Kagera Sugar vs Azam (Uwanja wa Kaitaba)
Oktoba 30- Villa Squad vs Ruvu Shooting (Uwanja wa Chamazi)
Oktoba 30- Mtibwa Sugar vs Moro United (Uwanja wa Manungu)
Novemba 2- Oljoro JKT vs Villa Squad (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid)
Novemba 2- Moro United vs Simba (Uwanja wa Taifa)
Novemba 2- Polisi Dodoma vs Yanga (Uwanja wa Jamhuri)
Novemba 2- Toto Africans vs Azam (Uwanja wa CCM Kirumba)
Novemba 2- Mtibwa Sugar vs African Lyon (Uwanja wa Manungu)
Novemba 2- Ruvu Shooting vs JKT Ruvu (Uwanja wa Mlandizi)
Novemba 3- Kagera Sugar vs Coastal Union (Uwanja wa Kaitaba)

LIGI DARAJA LA KWANZA
Mzunguko wa kwanza wa Ligi Daraja la Kwanza unamalizika wiki hii kwa mechi zifuatazo;
Kundi A
Oktoba 30- Morani vs Polisi Dar es Salaam (Uwanja wa Kiteto)
Oktoba 30- Transit Camp vs Burkina Faso (Uwanja wa Mkwakwani)
Oktoba 31- Temeke United vs Mgambo Shooting (Uwanja wa Mlandizi)

Kundi B
Oktoba 30- Mbeya City vs Small Kids (Uwanja wa Sokoine)
Oktoba 30- Majimaji vs Tanzania Prisons (Uwanja wa Majimaji)
Oktoba 31- Polisi Iringa vs Mlale JKT (Uwanja wa Samora)
Novemba 3- Polisi Iringa vs Small Kids (Uwanja wa Samora)

Kundi C
Oktoba 31- 94KJ vs Manyoni (Uwanja wa Mlandizi)

POULSEN vs WAANDISHI WA HABARI
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen atakutana na waandishi wa habari kuzungumzia maandalizi ya mechi dhidi ya Chad itakayochezwa Novemba 11 mwaka huu ikiwemo kutaja kikosi chake.

Tarehe: Oktoba 31, 2011

Muda: Saa 5 asubuhiMahali: TFF

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

1 Comments

  1. YANGA BOMBA - UHURU BRANCHOctober 30, 2011 at 11:04 PM

    ANGALAU SIKU HIZI TANZANIA HAIKO KWENYE KUNDI LA NCHI ZA CHINI KABISA KISOKA KAMA HIZO NNE ZITAKAZOANZA KUCHUJANA ILI KUINGIA KWENYE RATIBA KUU,ZAMANI NDIO YALIKUA MAENEO YETU HAYO

    MDAU WA BOMBA - USA

    ReplyDelete
Previous Post Next Post