JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limejipanga kuimarisha ulinzi na usalama katika pambano la soka kati ya Simba na Yanga utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Suleiman Kova (Pichani)amesema kuwa jeshi lake limejipanga kushirikiana na vyombo vingine vya dola ukiwa ni mkakati madhubuti utakaohakikisha mchezo kuchezwa kwa amani na utulivu.
Kova alisema udhibiti huo utakwenda sambamba na kuzuia vilevi uwanjani na vinywaji vingine vya chupa za vioo uwanjani siku ya mchezo huo na silaha kama kisu, panga na nyinginezo.
Aidha Kova alisema udhibiti huo kupitia kamera maalum za video zitakazowekwa ili kuweka kumbukumbu na kubaini matukio yote yatakayojitokeza uwanjani hapo kabla ya mchezo na baada.
Kova alisema utupaji wa chupa za vimiminika vya aina yoyote, mkojo haviruhusiwi na hatua dhidi ya vitendo hivyo zitachukuliwa hatua za kisheria.
Kova alisema ili kufanikisha ulinzi uwanjani hapo, atakayemuona anayevunja sheria atume ujumbe mfupi wa (sms) kwenye namba 0783 034224 ujumbe huu utaingia kwenye Computer ya Polisi ambayo itakuwa hapo na hatua zitachukuliwa mara moja.