WAMBURA AISHANGAA TFF

Na Makuburi Ally

MGOMBEA Uenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Mara (FAM), aliyeenguliwa, Michael Wambura, amesema anashangazwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumtaka apeleke rufaa yake Mahakama ya Usuluhishi wa Michezo ya Kimataifa (CAS), wakati yeye si mwanachama wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Akizungumza na Tanzania Daima, Wambura alisema, kwa mujibu wa Katiba ya FIFA, wanaotakiwa kupeleka mashitaka CAS ni Shirikisho, Klabu za Ligi Kuu na Vyama vya mikoa.
“Nimejipanga kutetea haki yangu, mwaka huu nina hakika mwelekeo utafahamika, kwa sababu haiwezekani kila ninapoomba uongozi nazuiliwa pasi na sababu za msingi,” alisema Wambura.
Wambura alisema, pamoja na TFF kukataa kupokea rufaa yake kupinga kuenguliwa kuwania nafasi hiyo, jana alilipa sh. 300,000 kwa ajili ya rufaa hiyo kwenye akaunti ya shirikisho hilo, huku akijipanga na Mwanasheria wake ajue cha kufanya.


Wakati TFF chini ya Katibu Mkuu wake, Angetile Osiah, likisema uamuzi wa kumuengua Wambura uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ndio wa mwisho, hivyo kama anaona hana hajatendewa haki aende CAS, Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi, Kamishna mstaafu, (CP), Alfred Tibaigana, ameagiza rufaa hiyo ipokelewe, jambo ambalo limekuwa gumu kutekelezwa.

1 Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 27, 2011 at 8:00 PM

    MICHAEL BWANA AKING'ANG'ANIA KITU...!SASA WEWE UMESHAAMBIWA THE DECISION IS FINAL UNANG'ANG'ANIA KUKATA RUFAA WANAKATAA HATA KUIPOKEA ETI UNAENDA KULIPIA BANK!UNALIPIA NINI SASA???HIVI MICHAEL ASIPOKUWA KIONGOZI WA MPIRA ANAKOSA NINI HASA,KWANINI ANALAZIMISHA KIASI HIKI,ANATAKA NINI NA AMEKIONA NINI HUKO NDANI AMBACHO SISI WENGINE HATUKIONI?KUNA DHAMBI MBILI ANAZO,MOJA KUTUMIA HATI YA UWANJA WA KARUME AMBAO NI MALI YA TTF AKIWA MADARAKANI KWENDA KUCHUKULIA MKOPO BINAFSI,HAPA NO UADILIFU,PILI KATIKA HARAKATI ZAKE HIZI HIZI ZA KUNG'ANG'ANIA MADARAKA ILI LAZIMA AWE KIONGOZI WA SIMBA AKAPELEKA MAHAKAMA MASUALA YA MPIRA!
    KIUFUPI MICHAEL UKO NJIANI KUPIGWA GLOBAL BAN NA FIFA KATIKA MAMBO YA MPIRA KAMA TFF WAKIPELEKA HABARI ZAKO KULE,WANAKUSTAHI TU,WE RUDI ZAKO KWENYE CRICKET KULE HAKUNA KELELE.

    ReplyDelete
Previous Post Next Post