UONGO MTUPU, BOBAN HAJAMPIGA OKWI-SIMBA





TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KATIKA baadhi ya vyombo vya habari jana na leo, kumeripotiwa taarifa za kuwapo kwa ugomvi baina ya wachezaji wawili wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi na Haruna Moshi Shaaban (Boban).
Ugomvi huo umeripotiwa kutokea mara baada ya pambano la watani wa jadi lililofanyika jana katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Vyombo hivyo viliripoti kuwa chanzo cha ugomvi huo ni madai ya hujuma na kutoaminiana ndani ya timu.
Kwa masikitiko makubwa, Simba Sports Club (SSC) inapenda kukanusha kwa nguvu zote kuwapo kwa ugomvi wa aina yoyote baina ya wachezaji au viongozi wa klabu mara baada ya pambano la jana.
Mara baada ya mechi, hali iliyotamalaki ilikuwa ni ya fadhaa na huzuni kwa wote wanaohusika na Simba, wakiwamo wachezaji na washabiki.
Habari hizo za ugomvi wa wachezaji ni uzushi unaoenezwa na watu wasioitakia mema SSC.
Kuna mambo mawili yanayoweza kubainisha kuwa habari hizo hazikuwa za ukweli. Kwanza, kwamba vipo vyombo vilivyodai kuwa Okwi alipigwa hadi kuvimba uso. Ukweli ni kuwa Okwi yuko salama, buheri wa afya na hajavimba popote mwilini mwake, achilia mbali usoni.
Pili, kuna magazeti yaliyoandika kuwa Okwi alipigwa vichwa vinne Boban kabla hawajaamuliwa. Mengine yakaripoti kichwa kimoja. Kuna redio imeripoti kuwa vilikuwa vichwa vitatu. Tukio moja, taarifa tofauti lukuki.
Kikubwa ni kuwa, hakuna mwandishi wa habari hata mmoja aliyeshuhudia tukio hilo na kulithibitisha pasi na shaka zaidi ya kusimuliwa na wale waeneza uongo.
SSC inashukuru kwa ushirikiano mzuri inaopata kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje.
Tunawaomba wana Simba wawe watulivu katika kipindi hiki na tujipange kwa ajili ya mechi yetu ijayo ya VPL dhidi ya Moro United. Kama tutashinda, tutaongoza ligi hadi mwakani.
Timu inarejea kambini leo tayari kujiandaa na pambano hilo la mwisho la raundi ya kwanza ya VPL.

Ezekiel Kamwaga
Msemaji
SSC

3 Comments

  1. YANGA BOMBA-UHURU BRANCHOctober 30, 2011 at 11:18 PM

    BWANA MSEMAJI KUMBUKA HABARI YA UKWELI HUWA HAIKANUSHWI..NAONA KIPIGO BADO KINAWALEVYA HIZO HABARI ZIMEPENYEZWA NA WACHEZAJI HUSIKA WALIOKUWEPO HUKO KWENYE DRESSING ROOM NA HAZINA CHEMBE YA SHAKA HUYO MVUTA BANGI WENU KAMPIGA OKWI SEMA KWA KUWA MNAMPENDA NA KUMUOGOPA KWA KUWA NDIO MUNGU WA SIMBA MNAMTETEA N KUJIFANYA HAKUNA KILICHOTOKEA,JE BWANA MSEMAJI ANAWEZA KUTUELEZA SABABU ZA MVUTA BANGI HARUNA KUTOPANADA BASI MAALUM LA WACHEZAJI NA BADALA YAKE KUPANDA TEKSI????KWANINI ALIFANYA HIVYO NA NANI ALIMRUHUSU KUFANYA UTOVU HUO WANIDHAMU MWINGINE,WADAU TUACHE KUMPENDA HARUNA KUPITA KIASI SISI NDIO TUMEMHARIBU NA KUMFIKISHA HAPO KUTOKANA NA KUMBEMBELEZA BEMBELEZA,KUNA WATU WALIJITOKEZA TENA WENGINE KWA KUANDIKA MAKALA KUMTETEA ALIPOHARIBU MKATABA ULAYA KWA SABABU ZA KIJINGA TU....AKIITWA NATIONAL TEAM AKIKATAA WATAJITOKEZA WA KUMTETEA,TUNAMUHARIBU HUYO MTOTO KWA KUMPENDA KUPITA KIASI,NI SAWA NA MTU MWENYE MTOTO MCHANGA ANAPOZIDISHA MAPENZI KWA HUYO MTOTO MPAKA ANAMZIBA ASIPATE PUMZI AKIDHANI NDIO KUMPENDA KUMBE ANAMUUA!!!BWANA KAMWAGA USIKUBALI KUTUMIKA TU NA MUAJIRI WAKO MASAIDIE HARUNA NA SIMBA PIA,ELEZENI UKWELI,HARUNA ANA MATATIZO,HUO NDIO UKWELI.

    MDAU WA YANGA BOMBA-MICHIGAN,USA

    ReplyDelete
  2. yani nyie bado wanaweweseka na kipigo!si tumeshasahau,tunasonga mbeeeeele!

    ReplyDelete
  3. eti "kama tutashinda tutaongoza mpaka mwakani" kweli bado mko kwenye hangover ya kichapo!

    ReplyDelete
Previous Post Next Post