Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu , Usuluhishi na Rufaa Baraza
la Michezo la Taifa (BMT) Alex Mgongolwa (katikati) akitoa tamko leo jijini Dar
es salaam la kumfungia maisha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania
Shaban Kashinde Bundala kutojihusisha na mchezo huo na mingine kwa kujihusisha
na usafirishaji wa watu nje ya nchi kwa kisingizio cha kuwa wanamichezo bila
kibali cha BMT. Wengine ni Msemaji wa BMT Maulid Kitenge (kulia) na Katibu Mkuu
wa BMT Henry Lihaya(kushoto)
Na Tiganya Vincent-MAELEZo-Dar es alaam
Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limemfungia maisha
aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Judo Tanzania Shaban Kashinde Bundala
kutojihusisha na mchezo huo na mingine kwa kujihusisha na usafirishaji wa watu
nje ya nchi kwa kisingizio cha kuwa wanamichezo bila kibali cha BMT.
Tamko hilo limetolewa leo jijini na Mwenyekiti wa Kamati ya
Nidhamu , Usuluhishi na Rufaa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Alex Mgongolwa
(katikati) wakati akiongea na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) mjini Dar es salaam.
Alisema kuwa Kamati hiyo imeridhika na yaliyobainika katika
sakata hilo
bila shaka yoyote kuwa Bundala amekuwa akijihusisha na usafirishaji wa watu nje
ya nchi kwa kisingizio cha kuwa wanamichezo kwa kisingizio cha kwenda kushiriki
mashindano yanayoandaliwa katika nchi mbalimbali bila kibali cha BMT.
Mgongolwa amesema kuwa BMT imebaini kuwa Bundala alikuwa
anajihusisha na mipango ya kusafirisha watu nje ya nchi kwa kisingizio kuwa ni
wanamichezo wanaokwenda kushiriki katika michezo iliyoandaliwa huko bila ruksa
wala kibali kutoka BMT huku akitambua ni kosa.
Alisema kwa mfano mwaka 2011 alisafirisha watu wapatao 27
akiwemo yeye mwenyewe mpaka Nairobi Kenya kwenda kuomba Viza za Ubalozi wa
Poland ambapo baadhi yao walinyimwa Viza baada ya kuwasilisha nyaraka bandia na
hivyo kusababisha Ubalozi kuwalisiana na Serikali juu ya uhalali wa shuguli za
Bundala.
Mgongolwa aliongeza kuwa mwezi Oktoba 2011 Bwana Bundala
aliwasilisha majina ya watu 18 katika Ubalozi wa ufaransa kuomba Viza ya
kuingia nchini humo hata hivyo baada ya kuchambuliwa ilibainika kuwa nyaraka za
majina ya watu hao nyingi zao zilikuwa batili na BMT aikuwa na taarifa juu ya
safari hiyo.
Aidha BMT inatoa tahadhari kwa vikundi na vyama vya michezo
kuacha kutumia michezo kama njia ya kufanya amambo yao mengine amabyo siyo ya kimichezo kwa
kutumia mgogo wa michezo.
Alisema kuwa hali hiyo inachafua sura ya nchi na kurudisha
nyuma maendeleo ya michezo nchini .
Wakati huo huo Msemaji wa BMT Maulid Kitenge alisema kuwa
Baraza hilo
linatarajia kujadili na kutoa uamuzi juu ya mgogoro uliodumu kwa muda mrefu
baina ya aliyekuwa Katibu wa CHANETA Anna Kibira na CHANETA.