KLABU ya soka ya Simba
imetishia kugomea kucheza mechi zake katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam , pia kuzuia wanachama wake kuingia uwanjani,
kutokana na uonevu wanaofanyiwa na Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) katika mchakato mzima wa mapato ya mlangoni.
Hatua hiyo inafuatia juzi TFF
kuikata Simba mgao wake wote wa shilingi mil.3.5 ilioupata kupitia mapato ya
mchezo wao wa ligi kuu baina yao
na Kagera Sugar ya Kagera kwa madai ya fidia ya shilingi mil.tano wanazotakiwa
kulipa baada ya wanaodaiwa mashabiki wa Simba kuharibu viti vya uwanja huo
katika mechi baina ya Simba na Kiyovu iliyofanyika jumapili iliyopita.
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage amesema leo kwamba
wanashangazwa na uonevu wa wazi unaofanywa na TFF , kwa kuwa uwanja huo si mali
yao na wamekuwa wakilipa fedha nyingi
kabla ya mchezo kama tahadhari kwa uharibifu wowote utakaotokea lakini
haijulikani fedha hizo zinakwenda wapi.
“Mfano mechi yetu na Kagera
Sugar juzi mapato yalikuwa mil.24 na
baada ya makato ya mamlaka mbalimbali zilibaki mil.7 na vilabu kugawana hivyo
kila timu kupata mil.3.5, huu ni unyonyaji kabisa kwani pamoja na vilabu
kugharamika kwa fedha nyingi kwenye maandalizi lakini mwisho wa siku wanakuja
kufaidika watu wasiochangia mapato yoyote,”Alisema
Aden anachotakiwa yeye na uongozi wake sio kulia lia bali wawape semina elekezi washabiki wao kukaa kistaarabu uwanjani,na waace mchezo wa kuonyesha furaha za ushindi kwa kung'oa viti kwani mwisho wa siku kunaigharimu club,zipo njia nyingo za kushangilia ushindi,yanga bomba wanaweza kuwapa somo la ushangiliaji kama wataombwa na uongozi wa simba kwa barua rasmi.
ReplyDeletemdau wa bomba,revere masachussetts usa