BENDI ya muziki wa dansi ya Mashujaa Musica imezidi kuibomoa bendi ya African Stars ‘Twanga
Pepeta’ baada ya kumyakua mnenguaji wake
mahiri,Lilian Tungaraza maarufu kama ‘Intanet’.
Meneja wa Mashujaa Band Maximilian
Luhanga alisema kwamba wamweamua kuwachukua wanamuziki hao ili kuimarisha bendi
yao katika
idara hizo na tayari wameshasaini mkataba wa kuitumikia
bendi hiyo kwa miaka miwili ambao onyesho la utambulisho linatarajiwa kufanyika
jumatano ijayo katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Hii ni mara ya pili kwa Mashujaa kuibomoa Twanga Pepeta
ambapo mapema mwaka huu ilimyakua mmmoja ya waimbaji mahiri, Charlz Gabriel ‘Chaz
Baba’.