NEW YORK, Marekani
RAPA Kanye West amebuni viatu vyake vya kike ambavyo
ataviuza kwa akina dada kwa kupitia Kampuni yake ya Dw kwa kushirikiana na
Collete ya Ufaransa ambayo imeshiriki katika maonesho yaliyopewa jina la Paris
Fashion Week mwaka 2012.
Viatu hivyo vya rapa huyo vinatarajiwa kuuzwa kati ya dola 6,000
au euro 4,420 kwa mujibu wa kampuni inayoletea kutoka Ufaransa.
Viatu vyake hivyo vinamng’aro ulionakshiwa kwa madini
mbalimbali, vikiwa vinapatikana katika maduka makubwa ya Harper Bazaar
Australia na Italia ambako ndiko kumebuniwa na mbunifu wa nchini humo, Giuseppe
Zanotti.
Rapa huyo
ambaye kwa sasa anajihusisha na masuala ya uajasiriamali wa urembo alionesha
kuvutiwa na mtindo ya onesho hilo la mwaka huu.