ONYESHO
maalum la utambulisho wa wasanii wapya waliojiunga na bendi ya muziki wa dansi
ya Mashujaa Band, mnenguaji Lilian Tungaraza ‘Internet’ na mpiga gitaa Ally
Akida linatarajiwa kufanyika KESHO katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Internet
aliyekuwa akifanya kazi katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Akida
aliyerkuwa mwanamuziki wa kujitegemea walijunga na MAshujaa wiki iliyopita
baada ya kusaini mktaba wa miaka miwili.
Mbali ya Mashujaa , onyesho hilo pia litapambwa na Machozi Band
inayomilikiwa na Mwanadada Lady Jay Dee ambapo kutakuwa na mambo mazuri ya
kuvutia.
“Si onyesho
la kukosa kwa mpenda muziki wa dansi kwani pamoja na utambulisho wa wasanii
wetu wapya, bendi hizi zinatarajiwa kukonga kwa nyimbo zake kadhaa sambamba na
shoo ya nguvu toka katika sdafu zao za unenguaji,”Alisema Luhanga.
Naye Lilian
akizungumzia hatua ya kuhamia kwake Mashujaa alisema kilichompeleka huko ni
maslahi mazuri mazuri anayolipwa kwa kazi yake sambamba na fedha ya kujikimu
kwa masuala mbalimbali ikiwemo matibabu, usafiri na nyumba.
Alisema
pamoja na hilo amekwenda huko kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi katika harakati
zake hizo za kusaka maisha kupitia muziki huku akiwaahidi mambo makubwa
mashabiki wa bendi hiyo na muziki wa dansi kwa ujumla.
Internet
amekuwa msanii wa pili kunyakuliwa na Mashujaa Musica hivi karibuni toka Twanga
Pepeta ambayo mapema mwaka huu ilimchukua mwimbaji Charles Gabriel ‘Charlz Baba’
kwa lengo la kuimarisha kundi lao.