Mchezaji wa timu ya
Simba mganda Emmanuel Okwi kulia akijaribi kumtoka mchezaji wa timu ya
Kiyovu ya Rwanda wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho katika ya timu
hiyo na Kiyovu ya Rwanda unaofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
Simba
imefanikiwa kuiondosha Kiyovu ya Rwanda magoli 2-1, magoli ya Simba
yamepatikana katika kipindi cha kwanza na yamefungwa na mshambuliaji
Felix Sunzu akipokea pasi nzuri, kazi iliyofanywa na mchezaji
Emmanuel Okwi wa Simba.
Timu ya Kiyovu imepata goli
lake la kufutia machozi katika kipindi cha pili cha mchezo huo, kwa matokeo hayo, Simba
imefanikiwa kusonga mbele katika michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho
barani Afrika,
Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia vilivyo wakati timu yao ilipokuwa ikichuana na timu ya Kiyovu ya Rwanda katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Barabi Afrika uliofanyika leo kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.