Timu ya Yanga kutoka Tanzania imepata
kichapo cha goli moja kwa bila na timu ya Zamalek ya Misri leo , katika
mchezo uliofanyika nchini humo jioni ya leo ikiwa ni michuano ya Klabu
Bingwa Afrika, wiki mbili zilizopita hapa jijini Dar es salaam Zamalek
iliilazimisha Yanga kwa kufungana goli 1-1 kwenye uwanja wa |Taifa kwa
matokeo ya leo ina maana Zamalek imeifunga Yanga magoli 3-1 na kuitupa
nje ya mashindano hayo