WAKATI kesho itashuka kwenye dimba la Taifa Dar es Salaam kucheza mechi ya ligi kuu bara dhidi ya Kagera Sugar ya Kagera, Wekundu wa Msimbazi Simba watamkoa mshambuliaji
wake Mwinyi Kazimoto ambaye alichanika nyama za paja katika mchezo wa kombe la Shirikisho (CAF) baina ya Simba na
Kiyovu jumapili.
Kutokana na maumivu hayo, itamlazimu Kazimoto kuwa nje ya dimba kwa siku kumi, hivyo
kuungana na majeruhi wengine Juma Jabu na Ulimboka Mwakingwe.