MKANDA wa ubingwa wa ngumi za kulipwa wa TPBO (Oganaizesheni ya ngumi za
kulipwa) unatarajia kuwaniwa April 9 mwaka huu Dar es Salaam.
Mkanda huo
ambao upo wazi utawaniwa na bondia kati ya Thomas Mashali na Selemani Galile
uzito wa kg 75 middle weight.
Akizungumza maandalizi yake
Galile alisema amejiandaa vyema kwa ajili ya kunyakua mkanda huo ambao upo wazi
kwa sasa.
"Naendelea kufanya mazoezi yangu kwa ajili ya kuwania mkanda
huu ambao ninaamini utaweza kunitambulisha ubora wangu katika tasnia hii ya
masumbwi,"alisema Galile.
Alisema kuhusu mpinzani wake Mashali hana hofu
naye kwa kuwa mchezo huo huamua nani mkali atakayetwaa ubingwa wakati wakiwa
ulingoni na si nje ya hapo na kwa sasa nimepata staili mpya za mabondia wa
dunia.
Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi
pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa
Kimataifa wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa
ajili ya kuwapa mabondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za
masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio,
Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye,Lenox Lewis,Evalnder Holfilder
na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao
ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya
utangulizi