WACHEZAJI wa zamani waliopata kuichezea
timu ya soka ya Simba, Zamoyoni Mogella ‘Golden Boy’ (kushoto) na Boniface
Pawasa wamewaasa wachezaji wa timu hiyo kuichezea timu hiyo kwa nguvu zote ili
kuiletea mafanikio.
Wakizungumza
katika hafla ya uzinduzi wa Simba Tv mwishoni mwa wiki iliyopita, Mogela na
Pawasa walisema mafanikio ya Simba yatapatikana kutokana na kujituma
kwao.Walisema kutokana
na timu hiyo kuwa na kila kitu ikiwemo kocha mzuri pamoja na wachezaji wenye
vipaji hawana budi kutimiza majukumu yao ipasavyo ili kuiwezesha timu hiyo
kufanya vema katika mashindano ya ndani na nje ya nchi.
“Nakumbuka wakati ninaichezea Simba miaka
ya nyuma kikubwa ilikuwa ni kutanguliza utashi wa kazi yangu hii pamoja na
maslahi ya klabu kwanza na ndipo mafaniko yalipatikana, hivyo nawaomba wadogo
zangu mtangulize maslahi ya Simba kwanza ili muweze kuwa na mafanikio,”Alisema
Mogella.
Mogella alisema
kwamba macho na akili za mashabiki wa Simba zipo mikononi mwao hivyo kufanya
kwao vibaya kutawaangusha pia Wanasimba wote na Taifa kwa ujumla.
Naye Pawasa
aambaye alipataa kuicheze timu hiyo katika miaka ya mwanzo mwa 2000 hadi 2005
alisema enzi zao walikuwa na kauli mbiu ya ‘Simba Kwanza’ na
kutokana na hilo waliweza kupata mafanikio.
Akiwa ni mmoja ya
wachezaji wa Simba walioweza kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri mwaka
2003, alisema anaaminani na timu hiyo kuweza kufika mbali katika michuano ya
kimataifa kutokanba na vipaji walivyonavyo lakini kikubwa zaidi ni wachezaji
wake kujituma.