Mkurugenzi
wa Ufundi na Afisa Maendeleo wa Shirikisho la Soka(TFF) Sunday Kayuni,akizungumza
wakati ufunguzi wa semina elekezi ya msimu wa mashindano ya Copa Coca Cola 2012
kwa Makatibu wa vyama vya Mikoa jijini Dar es Salaam jana
WADHAMINI wa Mashindano ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17,
maarufu Copa Coca Cola wanaratajia kutumia Sh zaidi ya bilioni mbili katika msimu wa mwaka huu.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya vinywaji Baridi Coca Cola, Tanzania, Evance Mlelwa alisema kila mwaka, wamekuwa
wakiboresha udhamini wa mashindano hayo.
Mlelwa
alisema hayo, wakati wa semina elekezi ya makatibu wa vyama vya soka vya
mikoa nchini, iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Alisema msimu uliopita kampuni hiyo ilitumia Sh bilioni 1.5 kwa ajili ya uendeshaji wa mashindano hayo.
Mlelwa alisema kamapuni hiyo inaingia mwaka wa sita kudhamini mashindano hayo, ambayo yamekuwa na mafanikio
makubwa.
Kwa upande wa Makamu wa Kwanza wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF), Athuman Nyamlai alisema kumekuwemo na changamoto kubwa katika mashindano hayo.
Nyamlani alisema moja ya
changamoto hiyo ni gharamu kubwa ya uendeshaji wa mashindano hayo, ambapo viongozi wengi wa mikoa wamekuwa wakilalamikia
udhamini ni mdogo.
Alisema pamoja na malalamiko hayo,
wadhamini hao wamekuwa wakiongeza udhamini wao kila mwaka ili
kukidhi matakwa ya mashindano hayo.
Nyamlani alisema kwa miaka
sita ambayo wamekuwa wakishirikiana na Coca Cola kumekuwa na mafanikio
makubwa katika kuendeleza soka hususan vijana.
Alisema kwa
suala la kugushi umri wa wachezaji limepungua kwa asilimia 95, baada ya
baadhi ya viongozi kufungiwa kujihusisha na soka.
Nyamlani alisema tatizo la kudanganya umri si la Tanzania pekee
bali ni la dunia nzima, lakini wataendelea kulikemea ili waweze kujenga
timu bora ya vijana itakayokuwa na mwelekeo wa
mbele.
Naye, Mkurugenzi wa Idara ya Michezo nchini, Leonald Thadeo
alisema mashindano hayo, yamekuwa na umuhimu mkubwa katika kuendeleza soka .
Thadeo aliwataka viongozi wa makatibu
wa mikoa kuwa na ubunifu wa kuandaa mashindano mbalimbali ambayo
yanaleta wadau pamoja.
Hata hivyo, aliwaomba wadhamini wa mashindano hayo kuona umuhimu wa kushirikiana na Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), katika kuhakikisha wanawaendeleza wachezaji wanaochaguliwa kuunda timu ya Taifa.
Mashindano hayo
yanatarajia kuanza Machi 31 mwaka huu, ngazi ya wilaya.