TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
YAH: TAARIFA
ILIYOTOLEWA NA MWENYEKITI WA KAMATI YA UCHAGUZI WA
Nimepokea taarifa za shutuma mbali mbali dhidi yangu zilizotolewa
na Bw Lyatu kupitia kwenye magaazeti
mbali kupitia kwenye mitandao pamoja na taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na Bw Lyato 6/3/2012, Awali ya yote ningependa watanzania wafahamu
kuwa Kamati hiyo ya uchaguzi ya TFF haijawahi kuwa huru na haijawahi
kufanya maamuzi ya haki dhidi yangu hata
mara moja, silazimishi wafanye hivyo ila katika kufuatilia haki kuna siku
ukweli utajidhihiri, labda niwakumbushe, baada ya uchaguzi 2004 kuisha ambapo
niligombea uraisi wa TFF na ndugu
L.Tenga ambapo tenga alishinda, baada ya hapo
mambo mengi juu yangu yalianza kujitokeza . Mwaka 2005 iliamuriwa
ufanyike uchunguzi wa mahesabu (Auditing) tangu nilipoingia madarakani wakati
huo FAT 2002,2003 na2004 kampuni iliyopewa kufanya ukaguzi huwo ilitoa orodha ya watu na malipo
mbalimbali ambayo hayakuambatana na hati za malipo zilizoidhinishwa “List of
Un approved vouchers with no supporting Documents” ambazo kimsingi ni kama
Hoja za kiukaguzi “Audit Querries” lakini haikuwa hivyo.
Tarehe 14/01/2006 TFF ilifanya mkutano wake mkuu wa
kawaida wa mwaka 2005, katika mkutano huo yaliwasilishwa mahesabu ya fedha
ambayo sio final Audited Accounts ambayo yalilenga kunidhalilisha na
kunishushia heshima mbele ya jamii, wakati huo mimi nilikuwa mjumbe wa mkutano
mkuu kupitia Klabu Simba kama mwenyekiti nilihoji utaratibu huo, taarifa hiyo
ya fedha ilitolewa ndani ya ukumbi bila wahusika nikiwemo mimi kupewa hoja
zinazonihusu na muda wa kujibu hoja hizo, Kwa kawaida mkutano mkuu hupelekewa
Taarifa kamali ya mahesabu iliyokaguliwa(Audited Accounts) baada ya kupata
majibu ya hoja za kiukaguzi kutoka kwa wanao husika jambo ambalo halikufanyika
kwenye hili. Baada ya kulalamika miezi mitatu baadae Tarehe 21/4/2006
niliandikiwa Barua na TFF yenye kumbukumbu TFF/ACC.06/2 yenye kichwa cha habari
“QUERIES ON PAYMENTS MADE TO YOU” yaani hoja zinazohusiana na
malipo yaliyofanya kwako, aidha barua hii ilinitaka mimi nikiwa mmoja wa watu
waliotajwa kwenye orodha ya watu waliolipwa malipo mbali mbali ambayo hayana
viambatanisho hivyo kupewa siku 30 kutoa
maelezo na majibu stahilli ili kufanikisha ukaguzi Maalum (SPECIAL AUDIT)
katika maenoa matatu(3):
1.
Kutathmini malipo
ambayo hayakuidhinishwa yaliyofanywa kwa viongozi wa FAT kamailivyo ainishwa
kwenye pendekezo 12. 2.
Kuanisha uhalali
wa madeni ya FAT mpaka 2004. 3.
Kutathmini
uhalali wa gharama za vifaa (Fixed Asset) zilizonunuliwa 2002-2004.
Tarehe 28/5/2006 niliandika maelezo na majibu yote ambayo nilitakiwa
kuyatolea maelezo, hoja zote zilizo
letwa kwangu zilijibiwa, sikupata maelezo mengine yoyote au maswali ya kutaka
ufafanuzi wa jambo lolote linalohusu ukaguzi.
Baada ya taarifa ya
ukaguzi maalum kutoka niliipata kwa njia zangu na kuisoma nikagundua kuwa
ukaguzi huo huenda ulinilenga mimi maana watu wote waliotoajwa kwenye ukaguzi
wa awali hawakutajwa tena, taarifa haikusema kama majibu yao yalitosheleza
matakwa yao na haikutaja kama majibu yangu hayakuwatosheleza na kukidhi
mahitaji yao. Katika Taarifa ya ukaguzi Maalumu (Special Audit) Kifugu 4.0 (a)
mkaguzi anasema viongozi wa FAT hawakuweza kupatikana kutoa maelezo kuhusiana
na hoja za kiukaguzi, hii inamaanisha kuwa majibu ya hoja niliyoyawakilisha TFF
tarehe 28/5/2006 hayakupelekwa kwa wakaguzi na kama mkaguzi alinihitaji basi
TFF ilimweleza sipatikani, ili report ionekane mimi ni mbadhilifu.
Kifungu 4.0(b) cha
taarifa hiyo pia kinasema kazi ya ukaguzi maalum imekuwa ngumu kwa kuwa
viongozi wa FAT hawajakabidhi ofisi hivyo nyaraka zinazohusiana na ukaguzi huo
kutokupatikana, hili ni jambo la kushangaza kwani nilkabidhi ofisi siku mbili
baada ya uchaguzi 29/12/2004 na wakati ukaguzi huo unafanyika mwezi 7-8/2006
iliisha pita miaka 2 swali linakuja kazi za TFF zilikuwa zinafanyikaje? Mimi
sikuwa mhasibu wa TFF ambaye nina tunza nyaraka za malipo, mhasibu wa TFF mpaka
hivi sasa yupo walishindwa nini kumuuliza? Ninachokiona mimi hizi zilikuwa ni
njama zilizofanywa kuficha nyaraka ili majibu yasipatikane ili nionekane
mbadhilifu na mwizi. Kifungu4.0(e) cha ukaguzi kinasema wamegundua makosa mengi
ya uandikaji wa kumbukumbu za mahesabu katika vitabu vya FAT, hiyo inamaanisha
kumbukumbu walizopatiwa hazikuwa sahihi na hivyo zilipaswa kuwekwa sawa kwanza
ili ukaguzi ufanyike jambo ambalo lilikuwa gumu kwa mkaguzi kwa kuwa nyaraka
nyingi hazikuweza kupatikana Mfano PV 5322 ya tarehe 22/6/2004 inaonyesha
malipo $ 3250 kwa ajili ya posho za safari kwenda Ruanda halafu maombi ya
idhini ya malipo iliyoambatanishwa nayo inataja PV 5322 Mr Wambura malipo ya
PTA’s for match kamisaa ya $350.
Ili
nionekane mbadhilifu Nimegundua maombi mengi ya uongo na kutunga ya idhini ya
malipo yameandikwa kuonyesha nilipokea malipo bila sahihi yangu ili mradi
yaonekane yalifanyika kwangu mfano 28/07/04
PV 5324.
Pamoja na Mkaguzi katika
repoti zake nyingi tangu ya awali kuitaka TFF iwasiliane na mimi ili majibu
yapatikane TFF haikuwahi kufanya hivyo kwa makusudi na kwa hila na nia mbaya na
mimi .
Mwaka 2008 niligombea
nafasi ya Makamu wa pili wa rais wa TFF katika mchakato huo jina langu
liliondolewa katika orodha ya wagombea, nilikata rufaa katika kamati ya Rufaa
ya TFF, katika moja ya hoja za TFF ni kwamba kuna hoja za kiuhasibu ambazo
sikuwa nimezijibu, hii ndio ilinionyesha ni kwa jinsi gani majibu yangu
yalifichwa na mkaguzi hakupewa, kwani mjibu yale yalikuwa na nakala 3 na
niliyakabidhi TFF 2006 iweje 2008 hawajayapata? , hivyo ikaamuliwa nipewe hizo
hoja nizijibu. Tarehe 1/12/2008 TFF iliniandika barua nyingine yenye Kumbukumbu
TFF/ADM/AP.08/07 yenye kichwa cha habari “YAH: HOJA ZA MAHESABU YA FAT
(TFF)” iliyosainiwa na Mtemi
Ramadhani, katika barua hii tff ilinitaarfu kuwa kamati ya Rufaa iliyoketi
tarehe 5/12/2008 imenitaka nijibu hoja za kiukaguzi kabla ya tarehe 10/12/2008
saa 6.00 mchana na ofisi itakuwa wazi kushirikiana na mimi kupata nyaraka hizo ili
zijibiwe, Jitihada za kupata nyaraka kutoka TFF ziligonga mwaba hakuna
aliyekuwa tarayari kutoa ushirikiano, 7/12/2008 nilimwandikia katibu mkuu wa
TFF nikimueleza juu ya malalamiko yangu kutokupa ushirikiano kutoka katika
ofisi yake, na kuomba nipatiwe nyaraka muhimu kabala ya tarehe 8/12/2008 saa
sita(6.00) mchana pamoja na nyaraka zifuatazo: 1.Nakala ya Ukaguzi
maalum(Special Audit Report) 2.Vivuli vya Nyaraka mbali zikiwemo receipt na
hoja za kiukaguzi
wa mahesabu.
Tarehe 8/12/2008 TFF kupitia barua yake TFF/ADM/GC.08/105
ilinijibu ikinitaarifu kuwa ofisi yake itanikabidhi nyaraka mbali mbali
zinazonihusu niende nizifuate, nilipozifuata kama barua katibu mkuu ilivyosema,
sikupewa ushirikiano wowote na niliyemkuta offisini nd Mtemi Ramadhani alikataa
kabisa kutoa ushirikano, niliiandukia TFF barua nyingine kuelezea kukosa
ushirikiano, tarehe 9/12/2008 siku moja kabla ya deadline nilipigiwa simu
niende kuchukua nyaraka, nilipewa vivuli vya profoma invoice, Accounts ledger
na barua moja ya kutoka kwa Marehemu Charles Masanja.
Tarehe 10.12.2008 kampuni ya Uhasibu na Ukaguzi ya E.K Mengesho
& Company ilitarifu TFF kwa niamba yangu wakabidhiwe vielelezo na hoja hizo za kiukaguzi, kampuni hiyo kupitia barua yake Kumb
MACO/AQR-MRW/12/08 iliitaka tff iwakabidhi nyaraka zifuatazo ili zijibiewe:
1.
Copy of complet
the complete Special Audit Report 2.
Copy of all
relevant documents touching Mr Wambura namely,2.1 Payment vouchers, 2.2 Invoices ,2.3 Receipts ,2.4
Personal Ledger,2.5 Journal Vouchers.
Barua hiyo haikujibiwa hadi hii leo, aidha nilichukua jitihada za ziada
kuwasiliana na wanasheria wa kampuni ya Uwakili
MSK LAW PARTNERS(ADVOCATES) nao waliwaandika TFF barua yenye kumbukumbu
MSK/TFF/08/01 yenye kichwa cha habari MICHAEL. R. WAMBURA –Audit Queries
kuwasisitiza TFF iliwaweze kunikabidhi nyaraka hizo bila mafanikio, hata hivyo
barua zote mbili hazikujibiwa hadi hii leo.
Pamoja na vikwazo vingi vya kupata nyaraka kutoka TFF nilioomba kamati
ya rufaa ikubali kupokea majibu ya hoja za kiuhasibu niliyoyatoa mwaka 2006 ili
yaweze kuongoza kikao, aidha kamati hiyo ilikubali na kupitia hoja mbalimbali
na kuridhika kuwa sikuwa na hatia ya ubadhilifu kama pingamizi
lilivyowasilishwa, aidha sababu ya kuondoa jina langu ni waswasi na suala la
Uadilifu (Intergrity) wa kuwa kampuni MIN INVESTMENT PROMOTION CO iliyofanya
biashara na TFF ilikuwa inamilikiwa na Mimi Michael Wambura, ukweli ni kwamba
kampuni hii inamilikiwa nd Josea Samuel kama inavyoonyesha katika Extract From
Register No 93017 ya Msajili wa Makampuni, Mnamo tarehe 10/12/2008 Bw Josea
aliiandika TFF barua akiambatanisha na vivuli vya Cheti cha Usajili akiitarifu
TFF kuwa yeye ndie mmiliki halali wa Kampuni hiyo na ni yeye ndiye aliefanya
biashara na TFF na kama kuna maelezo ya ziada yuko tayari kufiki pindi
wakimhitaji, Kwa kuwa TFF walikuwa na agenda ya Siri juu yangu waliamua
kuificha kamati ya rufaa juu ya taarifa(barua)hiyo na hatimaye kamati ya rufaa kuondoa jina
langu kwenye uchaguzi huo kwa sababu ambazo sio za kiubadhilifu.
Katika
kuhakikisha majibu yanapatikana na kuweka wazi juu ya suala hili, na kama TFF
inanituhumu kwa ubadhilifu ni kwanini nitumie nguvu zote hizo kupata nyaraka
ili nipate kujibu hoja zao? Kulikuwa na sababu gani niwaandikie TFF barua 3 na
nyingine kutoka kwenye makampuni ya ukaguzi na hata kutoka kwa wnasheria nabado
walishindwa kunikabidhi hizo nyaraka hizo hata kujibu barua? Ununuzi wa
Samani za Hostel Mwaka 1998 Fifa kupitia mradi wa FIFA Goal project
iliipitisha Tanzania kuwa moja ya nchi wanachama wa Fifa ambao wangepatiwa
mradi wa mendeleo katika awamu ya kwanza, Msimamizi Mshauri(consultant) MD
Consultancy-architect aliteuliwa kusimamia mradi huu, mpaka 29/12/2001 uongozi
mpya unaingia madarakani ujenzi mradi huu uliukuwa haujaanza kutekelezwa, aidha
sababu zilizoleteleza ucheleweshaji pamaoja na nyingine ilikuwa,
1.
Kuwasilishwa kwa
mapendekezo ya kubadili mchoro uliokuwa tayari umeidhinishwa na fifa kutoka
Hostel ili ujengwe uwanja wa mpira (Stadium)
2.
Kuchelewa
kupatikana kwa vibali pamoja na hati mbali mbali zinazoonyesha manispaa husika
iliridhia ujenzi huo,
3.
Kujua mmiliki
halali wa karume Staduim
4.
Makandarasi
kuandika maakadirio ya ujenzi kwa kutumia TSHs badala ya UDS($) Mwaka 2002
tulianza kusimamia ili kuhakikisha mradi huo unaaza kwani baadhi ya nchi
zilikuwa zimeisha kamilisha awamu ya kwanza na kuanza kuitumia. Wakati mradi
huo unaidhinishwa na FIFa, viwango vya kubadilisha fedha (Exchange Rate)
itakuwa ni sh 436 kwa dola mpaka mradi utakapo kamilika ili kuondoa uwezekano
wa mradi kushindwa kuendelea. Mwaka 2004 wakati mradi unakaribia kufika tamati
ilioneka kuwa gharama za mradi ziliongezeka
na FAT haikuwa na uwezo wa kulipia, tarehe 7/7/2004, Fifa ilihamisha
kiasi cha Dola $71,590.00 kutoka kwenye Accounti yetu ya FAP(Financial Assistance
Programme) na kuifanya akaunti hiyo kubaki salio sufuri, uamuzi kama huo
ulifanywa na fifa na mwanachama alikuwa anataarifiwa kwa kuwa malipo yalifanywa
na wao moja kwa moja. June 2004 mradi ulikuwa umefikia hatua za mwisho
kukamilika lakini katika BOQ(bills of Quantity) haikujumlisha Vifaa vya Hostel
Pamoja na ukuta wa kuzunguka eneo lote la karume,na kwa kuwa jambo hilo
halikuwemo kwenye mradi mshauri ujenzi alishauri zitafutwe hela kwa kuwa mradi
huo ni mwingine tofauti na wa awali. Msimamizi wa Maendeleo wa kanda yetu nd
Ashford Mamelodi alipokuja alikuta na kusema haiwezekani mradi ukazinduliwa
katika hali hiyo,hivyo aliagiza yatafutwe makampuni yanayoweza kufanya kazi
na yeye atashawishi fifa igharamie kazi hizi
1. Kujenga uzio(ukuta)
2.
Kusupply furnitures za hostel Makampuni mengi yalikuwa hayapendi kufanya kazi
na FAT/TFF kwa kuzingatia rekodi zake za fedha na ulipaji wake wa madeni,
Makampuni machache yaliweza kukubali kufanya biashara na FAT tena kwa gharama
kubwa kufidia muda na hasara nyinginezo ambazo wangeweza kukutana nazo
,makampuni kadhaa na yalileta Makisio ya gharama zao.Tulizipeleka FIFA, Nd
Mamelodi alipokuja alikutana na wawakilishi wa makampuni hayo na alikubali kuwa
atawalipa moja kwa moja. Mjenzi wa ukuta alilipwa moja kwa moja baada ya
kumaliza kazi na kuikagua Malipo ya zabuni ya vifaa vya hostel yaliletwa FAT
kwa kuwa sehemu ya fedha tulizoomba zingetusaidia kuiweka kambini na kuisafirisha Serengeti Boys na twiga Stars
kwenda Zimbabwe na Kigali. Lilikuja wazo la kununua Basi ili leweze kusaidia
timu zetu za Serengeti na Twiga kusafiri mara kwa mara kwa kuwa basi lilokuwepo
la FAT lilikamatwa na kupigwa mnada kutokana na madeni ya FAT ya mwaka
2000-2001, hivyo tulikubaliana katika $ 25,000/ zilizokuwa zimekuja tutoe Usd
10,000.00 ili kufanya malipo ya awali ya kununua Basi, kwa kuwa Fedha hizo
zinatoka FIFA ilikuwa lazima Mwenyekiti wa FAT aidhinishe kwanza ndio hatua
nyingine ifanyike kama inavyoonekana kwenye PV 5324 ya tarehe 29/7/2004 na
barua ya mwenyekiti kwa wakaguzi, mpango wa kununua basi ulishindikana kwa kuwa
FIFA iliagiza mzabuni alipwe pasipo maelezo mengine hivyo salio lililobaki la
USd 8,400.00 lisingeweza kununua basi hivyo zilihamishiwa kwenye matumizi ya
maandalizi ya timu ya Serengeti Boys
kwenda Ruanda kwa basi la kukodi na posho na Twiga stars kucheza na Zimbabwe
ikiwa ni usafiri na posho zao, kumbukumbu za malipo na matumiz yako kwa
mhasibu.
Kwa mujibu wa katiba ya
FAT ibara 42(3) (e)&(k) katibu mkuu ndiye Afisa mhasibuwa chama (Accounting
Officer) na atabuni njia mbalimbali za
kuongeza mapato ya FAT hivyo mamlaka yalikuwa yaniniruhusu kufanya na kuhamisha
mafungu ya fedha(Realocation of Funds) kutoka katika kifungu cha matumizi
ya kununua basi na kupeleka katika
matumizi ya timu za Taifa.
Tuhuma
zote alizozitoa Nd Lyato kuhusu ubadhilifu
zilitolewa pia, lakini kamati ya rufaa chini ya JAJI Mkwawa ili iliona sikua na hatia nazo na ushahidi
wake unaweza kupatikana katika kumbukumbu za majadiliano (Proccedings),pamaoja
na maamuzi yaliyotolewa hayakuwahi kunitaja mimi kuwa mbadhilifu au mwizi ,
hata kamati ya Uchaguzi chini ya Ng Lyato katika chaguzi 2 ambazo ni za Simba
na Mara (FAM) katika barua zake haikuwahi kutaja kuwa jina langu linaondolewa
kutokana na Ubadhilifu jambo linaloonyesha kuwa maneno aliyo yasema Lyato kwa
waandishi wa habari ni yake binafsi na sio ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF.
Ninapenda kumfahamisha bwana Lyatu Katiba ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema “ mtu hawi na hatia mpaka atakapo tiwa
hatiani na Mahakama” hivyo kuendelea kunizuia kugombea kwa mambo ya kufikirika
na ya kizushi ni kinyume na sheria jambo ambalo huenda likahitaji mkono wa
mahakama kutafsiri ,
Bwana
lyatu alijua mimi ni mbadhilifu ni vipi
nilipogombea uongozi wa FAM(Mara) alisahau kutumia kigezo hicho kwani sababu
pekee iliyotolewa na kamati yake ilikuwaa ni mimi kuipeleka Simba Mahakamani,
lakini hata kama ni kosa adhabu yake ni nini na imetajwa kwenye kifungu kipi
cha kanuni na Katiba ya TFF? Ni wazi
bwana lyatu amejazwa jazba na upepo hata kutumia maneno ambayo kwa mtu
anayefikiri kwa kutumia ubongo asingeweza kuyaandika ni wazi bwana Lyatu
ameingia kwenye siasa za Uchaguzi wa TFF 2012,hivi sasa imegundulika kuna
binadamu wawili (ufaransa na Uingereza) wamezaliwa na wanaishi bila ya kuwa na
ubongo. Napenda kumhakikishia bana Lyatu umri wa kugombea uongozi TFF ni miaka
18 ambayo mimi niliisha ipita na hata kama ningechaguliwa leo ukomo wa uongozi
wa TFF ni miaka 70 kwa mantiki hiyo sina sababu ya kudanganya umri,mimi
nimezaliwa hospitali hivyo nina cheti cha kuzaliwa, nina passport, kadi ya
kupigia kura nimesoma shule kuanzia Msingi, sekondari na Chuo kikuu DSM(UDSM)
ambapo kumbukumbu zangu zote za kuzaliwa zinapatikana, kwa kuwa nakala za form
hizo sijaziona siwezi kukubali au kukataa tofauti iliyojitokeza na kama ipo
itakuwa ni kosa la bahati mbaya amboyo sikuidhamiria lakini pia nitapenda nione
nakala halisi, mtu anayedanganya umri ni Yule ambae atakaefaidika kwa kufanya
udanganyifu huo, iwapo sifa za kikatiba ni miaka 18 na mimi sina nikajaza hivyo
hiyo itakuwa udanganyifu lakini kama nimeipita na nikaandika tofauti na bado
ninakidhi matakwa ya kikatiba hapo nitakuwa sikudanganya umri bali nimekosea
kujaza umri wangu mtu anayedanganya kama ambavyo nilikuandikia kuwa Katika
wilaya za Temeke Kinondoni na Ilala kuna viongozi waliochaguliwa hawana elimu
ya kidato cha Nne kama kanununi za TFF unazodai anazisimamia zinavyosema na
huku akiendelea kuwa bubu na kiziwi huku sauti na masikio kufunguka suala
linapokuwa linapomuhusu Wambura, Kwa kuwa hakuwa na nia njema na mimi, hata
kanuni ndogo ya haki za binadamu ya haki ya mtu kusikilizwa(right to be heard)
aliipuuza, kwani angeniuliza kuhusu utata huo angepata hasara gani? au
angalichelewa kuongea na waandishi? .
Napenda kumkumbusha Lyato niliwahi kusema hawezi na hata kaa hata siku
moja kunitendea haki, kwa mantiki hiyo nisingeweza kudanganya umri ,
ninachopenda ieleleweke ni vizuri kazi za watu zikabaki ofisini na mambo ya
kijamii na kibinafsi (social and personal issues) zikabaki mitaani kwani
unaweza kumfikira mtu na kumhukumu mtu kwa asilo litenda, kila wakati haki si
tu itendeke lakini ionekana kutendeka “justice must not only be done must
seen to be done’’ lazima maamuzi yafanyike posipokutilia chembe ya
shaka.
Kamati ya Uchaguzi ya TFF bila kuheshimu
kamati ya Rufaa ya TFF imeanza kuandikia mikoa wanachama wa TFF kupinga maamuzi
ya Kamati ya Rufaa ya TFF yote hani kisa maamuzi yale yalimsaidia Wambura na kwa kuwa mwaka huu kuna uchaguzi
mkuu wa TFF, aidha kamati hiyo imeamua kunyakua madaraka ya kuwa msemaji wa TFF
bila kujali athari za kisheria zinazoweza kuikumba tff kutokana matamshi na
maamuzi ya kamati hii, ni wazi kamati hii inanyakua mamlaka ya kikatiba ya
usemaji ya Rais na Katibu wa TFF, Humu duniani kuna aina nyingi za walevi
wengine pombe wengine madaraka na wengine huwa mbumbumbu wa sheria na mambo
mengine lakini hawataki waelimishiwe,
Mwl Nyerere alisema ni bora ukawa mjinga kulikoni mpumbavu maana mjinga
anafundishika, hivi upeo wa bwana Lyatu kuelewa kuwa Kamati ya Rufaa ni supreme
Organ(ni chombo cha cheye mamlaka ya juu) ndani ya TFF umeishia hapo? Ni kweli
wafanyakazi wanatakiwa kupelekwa kozi mara kwa mara lakini kwa TFF kumpeleka
Lyato kwenye hili itakuwa Ufisadi, hivi lyatu na kamati yake wanajua na
kufahamu Sheria kulikoni Prof Mgongo Fimbo? Wanaufahamu wa masuala ya utawala
wa michezo kuliko KIPINGU, TANDAU, Mhe MISANGA na Kamanda RWAMBOW,? Nikisema huu ni ulevi
sitakuwa nimekosea, ninachomshauri Nd Lyatu awaombe radhi watu hawa na ajiuzulu
kwani yeye amekuwa mzigo mkubwa na kusababisha majeraha na madonda makubwa
katika mpira wa Tanzania, kwani TFF na wadau wote hawazungumzii tena mpira bali
uchaguzi za TFF.
Kuhusu swala la kwenda CAS napenda nimkumbushe
bwana Lyato kwa kuwa yeye ni mbumbumbu wa sheria (ignorant in Law) maamuzi
yakiisha fanywa na chombo cha juu yanakuwa Binding to the parties(yanafunga
pande zote) ila yule ambaye anadhani
hakuridhishwa nayo ndie anayepaswa kukata rufaa kwa chombo cha juu zaidi,
maamuzi ya Kamati ya rufaa yalikuwa upande wangu(in my Favour) hivyo siwezi
kukata rufaa CAS ila kwa kuwa wewe hukuridhika namshauri uende huko ili upate
haki unayoitafuta na kwa kuwa hakuna chombo cha juu kilichotoa uamuzi tofauti,
maamuzi yanabakia valid mpaka hapo yatakapo tenguliwa, ni jambo la ajabu uamuzi
uliotenguliwa ni wa kamati yake halafu anatangaza kutokutambua, njia nzuri ya
kupinga maamuzi ni kukata rufaa sio kutotambua na kuifanya kamati ya rufaa
kichekesho kwa kuandika barua mikoani nakuikashifu.
Kwa mujibu wa mtiririko wa vyombo vya haki katika
katiba ya TFF inaanza Kamati ya Nidhamu,kamati ya Rufaa na Mahakama ya
usuluhishi ya Michezo, Kanuni zinaundwa ili kurahisisha utekelezaji wa katiba
hivyo kanuni haiwezi kuipinga katiba, Katiba ya TFF inasema Maamuzi ya kamati
ya Rufaa ni ya mwisho na hayatajadiliwa na chombo kingine chochote isipokuwa
CAS, wakati mamlaka ya kamati ya uchaguzi kuwa mwisho sio ya kikatiba ni ya
kikanuni ambayo yanatungwa na Kamati ya utendaji ya TFF ila katiba inatungwa na
kupitishwa na mkutano mkuu hivyo kwa Bw lyato kuipinga maamuzi kamati ya
rufaa hii inaonyesha ni jinsi gani
mawazo yake yamekosa nuru na
yamefubaa kutokana na upofu wa fikra
sababu tu ya kujaribu kulinda maslahi yake na ya wenzake ili kiongozi
wanayemtaka aweze kuchaguliwa ili
waendelee kuwa na nafasi ya kulivuruga soka la Tanzania.
Bwana lyatu alikuwa mwenyekiti kamati ya kuchunguza mazingira na
sababu zilizopelekea Serengeti Boys 2005 kuondolewa mashindanoni kama alijua
kuna CAS na Tanzania ilikuwa na uewzo wa kushinda rufaa kama walivyo kata CAF
ni kwanini aliacha nafasi ya Tanzania ikapotea bure na Tanzania kifungiwa miaka
2, ili hali anajua pahali kwa kukatia
rufaa ? hiyo ilitosha yeye na kundi lake kujiondoa TFF kwani kwa Tanzania
kufungiwa mashindano ya U17 kumeliumiza sana soka la Tanzania
Haikuwa nia yangu kutoa
maelezo yote haya ila nadhani wakati mwingine mototo akipaliwa ukimgonga
ngongoni maisha yanaanza upya kwa gharama nafuu, hivyo nimesema haya labda
bwana Lyatu na kundi lake watapata ufahamu bila TFF kutumia fedha kwa ajili ya
semina, ninapenda kusisitiza ni “kheri kuwa mjinga kuliko mpumbavu”(Nyerere
J.K).
Ninapenda kusisitiza kwakuwa tuhuma za bwana Lyatu zinazotokana na
hoja za kiuhasibu(Audit Queries) ambazo
zote ni za uongo zenye nia ya kunifanya nipoteze hadhi mbele ya jamii aidha
napenda kumhakikishia Nd lyato hili halitaniziba mdomo tutaendelea hadi
wababaishaji mtakapo rudi mlipotoka, aidha ninapenda kumhakikishia bw lyatu
katika uchaguzi 2012 utakapotangazwa nitachukua form na kugombea katika nafasi nitakayo iona ni mwafaka kwangu
bila kujali hila ghilba na fitna anazoniwekea, aidha kama yeye anavyodai ni muadilifu ni vizuri kutumia fursa hii
aliyopendelewa kushughulikia Suala la wilaya za DSM kwani kuna fununu kuwa
amepewa au amepokea zawadi/ahadi ili suala hili lipite katika mazingira ya
upendeleo kwani baadhi ya viongozi wa TFF ni
maswahiba na ni washiriki wa kambi moja ya uchaguzi ya TFF.
Ninamtaka bwana lyato awaombe msamaha watu wa Mara kwa
udhalimu wa kuingilia mchakato wa uchaguzi huku akishindwa kuweka wazi mgongano
wa kimaslahi na baadhi ya wagombe jambo linalopelekea kutilia shaka uadilifu
wake. Ninapenda pia kuwapongeza wana CCM wenzangu wa jimbo la ukerewe walioona ndugu lyato
hafai kuwa mbunge wao kwa kumyima kura 2010 , kwani kuwanyima kura watu wenye
uwezo kama balozi Kamanda, Mhe Mongela, na kumchagua kiongozi kama lyatu
ingekuwa ni hasara ambayo wana ukerewe na taifa kwa ujumla tungejutia kwa muda
mrefu kama kwenye mpira tunavyojuta. Mwaka 2008 ulikuwa ni mwaka wa uchaguzi
mkuu wa TFF ambapo tangia mwaka 2007 maandalizi ya wagombea yalianza mimi ni
likuwa ni mmoja wa watu waliotangaza azma yangu ya kugombea tena katika
uchaguzi mkuu wa TFF. Mwaka huo huo 2007 nilioonyesha nia ya kugombea tarehe
21/12/2007 TFF ilifungua jarada la malalamiko
kumb CD/IR/5110/2007 kwa Jeshi la Polisi kuwa kati ya 2002-2004
kulitokea ubadhilifu katika ofisi za
FAT na mimi Michael Wambura nikiwa
mtumishi wa FAT/TFF, Uchunguzi na upelelezi ulifanyika pamoja na kukusanya
vielelezo na maelezo ya mashahidi mbali mbali na jeshi la polisi , hatimae
jalada lilipelekwa kwa Mwanasheria mkuu wa serekali mwenye mamlaka ya kupitia
na kusoma kuona kama kuna kesi ya kujibu dhidi ya mtuhumiwa . Tarehe 26/10/2011
jeshi la polisi kupitia barua kumbu DSM/ILAL/CD/B.I/I/VOL.XI/50 iliyosainiwa na
Mkuu wa upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Ilala nd D. Nyanda-SSP ikiwataarifu
TFF juu ya matokeo ya uchunguzi wao na maelekezo ya mwanasheria mkuu wa
serekali ya barua kumb J/DSM/ILA/113/11 ya tarehe 1/4/2011 kama ifuatavyo
“Baada ya
mwanasheria wa serekali kulisoma jalada hili aliridhika kuwa mtuhumiwa MICHAEL
WAMBURA hakuwa na kesi ya kujibu dhidi ya tuhuma hizo, Barua ya mwanasheria wa
serikali Yenye kumbukumbu J/DSM/ILA/113/11
ya tarehe 1/4/2011 yahusika, Kwa
barua hii jalada la kesi limefungwa”
Kwa kuzingatia mlolongo
mzima na mchakato mzima wa ukaguzi wa mahesabu ya TFF pamaoja na vikwazo vingi
mbali mbali kutoka TFF tangu 2005 hadi 2012(miaka 8) ambavyo kimsingi vililenga
kunichafua na kuniharibia jina ili nisiweze kugombea uongozi na hatimae kuonekana mhalifu mbele ya jamii
ni wazi vilifanywa kwa malengo Fulani ya watu Fulani kwa hila. Matokeo ya
kamati ya Rufaa ya TFF mwaka 2008 hayakuniona mie mbadhilifu au mwizi, matokeo
ya uchunguzi wa polisi na maelekezo ya mwanasheria mkuu wa Serekali yanatoa
picha kamili ya Usafi wangu katika utendaji ambao kundi Fulani kwa maslahi yao
wanajaribu kunifanya nionekane sifai, swali ninalojiuliza ilikuaje wakapeleka malalamiko
polisi ya ubadilifu mwezi wa Dec 2007 na mimi kupewe hoja za kiuhasibu kujibu
Dec 2008? Mwaka mmoja baadae, ni wazi kesi hiyo ilifunguliwa kwa hila na kwa
manufaa ya watu Fulani.
nipenda watu wafahamu
wakati mwingine haki haipatikani kwa urahisi ni lazima uipiganie sio tu kwa
ajili yako ila pia kwa ajili ya watu wengine wanao weza kudhulumiwa haki yao
Ninamtaka ndugu lyato nani ya Siku saba(7) aniombe radhi kwa maneno aliyoyasema
juu yangu kupitia utaratibu ule ule alioutumia kunikashifu na kusema maneno ya
Uongo kinyume chahapo nitachukua hatua za kisheria juu yake, aidha ninatafakari
njia muafaka za kisheria zakufuata ili jambo hili lifike mwisho.
Katibu Mkuu (mstaafu)
FAT/TFF
MICHAEL RUDI KWENYE CRICKET NDUGU YANGU AMBAKO NAKO UADILIFU NADHANI UNAHITAJIKA PIA...!
ReplyDeleteHAKUNA ANAYEWEZA KUKUTAKASA UKARUDI KWENYE MPIRA,UNAPOTEZA MUDA.
MBONA WEWE ULIWAHI KUGOMBEA UKATIBU UENEZI WA CCM DAR NA KUSHINDWA NA HAJI SUNDAY?INA MAANA WATU WAWAPONGEZE WANA CCM DAR KWA KUKUNYIMA KURA AU?
NA PIA WEWE SI UMEWAHI KUGOMBEA UBUNGE HUKO KWENU AMBAPO PIA KATIKA UCHAGUZI WA NDANI WA CCM KURA HAZIKUTOSHA,VIPI TUWAPONGEZE WANA CCM AGAIN KWA KUKUNYIMA KURA KWA KUKOSA UADILIFU AU?
MDAU WA BOMBA.REVERE,BOSTON,MASACHUSSETTS.