Na Dina Ismail
PAMOJA na uongozi wa
klabu ya soka Simba kukanusha kwa nguvu zote kuwepo kwa mgomo wa wachezaji,
ukweli ni kwamba kuna mgomo wa chini chini unaendelea ndani ya timu hiyo.
Habari za ndani za klabu
hiyo zinaeleza kwamba licha ya kambi kuanza juzi katika hoteli ya Bamba Beach
iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kuna baadhi ya wachezaji hawakuripoti
kwa sababu tofauti lakini ukweli ni kuwa wanashinikiza kulipwa fedha zao.
Taarifa zinaeleza kuwa
uongozi uliahidi kuwapa kiasi cha shilingi mil.30 kama wangeshinda mechi yao yao
ya kwanza ya kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Es Setif ya Algeria jumapili
iliyopita na ambapo Simba ilishinda mabao 2-0.
Hata hivyo uongozi
uliwapatia wachezaji hao shilingi milioni 15 tu tena ambazo zinadaiwa kutolewa
na mmoja ya wadau wa timu hiyo Azim Dewji kama motisha ya wachezaji hao
kuifunga Es Setif, hali ambayo haikuwapendeza wachezaji wa timu hiyo na kuamua
kuendesha mgomo.
Imedaiwa kuwa kuna
baadhi ya wachezaji wameripoti kambini lakini mgomo unaendelea chinichini huku
wakiapa kutojitum akatika mechi yaop ya ligi kuu dhidi ya African Lyon mwishoni
mwa wiki kabla ya kufanya hivyo katika mchezo wa marudiano dhidi ya Es Setif
wiki ijyo.
Akizungumzia hilo, ofisa
habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alikanusha kuwepo kwa mgomo na kudai kuwa
taarifa hizo zinaenezwa na watu wasioitakia mema klabu hiyo ambayo kwa sasa ipo
imara.
Alisema wachezaji ambao
hawakuripoti kambini jana kila mmoja alikuwa na sababu za msingi zilizomfanya
asiripoti kambini ambapo wengi wao waliripoti jana.
“Kuna watu wanataka kutuvuruga
katika kipindi hichi ambacho Simba ipo makini zaidi katika mashindano
muhimu….suala la wachezaji kudai posho za mchezo halina ukweli wowote kwani
walishalipwa kinachostahili,”alisema Kamwaga.
Kamwaga aliongeza kuwa mkataba wa Simba hauelezi kuwa mchezaji
anatakiwa kulipwa kwa mechi za kimataifa hivyo hata fedha walizowapa ilikuwa ni
sehemu tu ya kuwatunuku kutokan na kujituma kwao lakini hazimo ndani ya
mkataba.
FRIENDS OF SIMBA HUWA HAWAPENDI MAFANIKIO YA SIMBA AMBAYO WAO HAWAJASHIRIKI KUYALETA,ALWAYS WANAPENDAGA WAONEKANE WAO NDIO WAO NA BILA WAO HAKUNA MAFANIKIO SIMBA,HIVYO YANAPOTOKEA MAFANIKO NDANI YA SIMBA AMBAYO HAYAKUWAHUSISHA WAO HUWA WANATAFUTA KILA MBINU KUIVURUGA TIMU KWA KUWATUMIA WAANDISHI WA HABARI NA WANACHAMA WANAOJIITA MAARUFU,NAWAPONGEZA SANA KINA ADEN KWA KUWADHIBITI ANGALAU SO FAR,YOTE NI KWA KUWA ADEN NI MTU WA MJINI,FRIENDS WENGI NI WA TU WA KUJA TU AMBAO WALIINGIZWA SIMBA NA MZEE WA TANDAMTI KARIAKOO NDUGU YANGU KD..!
ReplyDeleteSAYZ MDAU WA BOMBA,REVERE,BOSTON,MASACHUSSETTS.