SASA NI ZAMU YA WAKAZI WA DAR KUAMBULISHWA MSANII MPYA WA MSONDO NGOMA
byANID UPDATES-
0
BENDI
kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo ngoma inatarajia kutoa burudani katika jiji
la Dar es Salaam kwa ajili ya kumtambulisha mwana mziki wao mpya Shabani
Lendi. Akizungumza Dar es Salaam Leo, Msemaji wa bendi hiyo Rajabu
Mhamila 'Super D' alisema, baada ya kuwa Zanzibar na kutoa burudan kwa
kumtambulisha Msanii huyo.Sasa
imepanga kumtambulisha siku ya Alhamisi ambapo watakuwa Kilimani Pub,
Stakishari,Ijumaa Lidaz Clab, Kinondoni, Jumamosi TCC Klabu na Jumapili watakuwa
katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kwa ajili ya kumtambulisha Kikamilifu
msanii huyo.Super D amewataka wakazi wa Dar es
Salaam na Mikoa ya Jirani kuhudhuria kushuhudia burudan hiyo watakayoitoa ikiwa
ni pamoja kusikia nyimbo zao mpya ambazo ni miongoni mwa nyimbo zitakazo kuwa
katika albamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja kusikiliza nyimbo zao za
zamani.
Alizitaja nyimbo hizo mpya kuwa ni Suluu ya Shabani Dede,Nadhiri
ya Mapenzi ya Juma Katundu, Mjomba, Dawa ya deni kulipa na lipi jema ambapo
albamu hiyo inatarajia hivi karibuni.