Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya
miaka 17 (Serengeti Boys) leo (Machi 2 mwaka huu) imeanza kambi yake ya wiki
moja ambayo hufanyika kila mwezi jijini Dar es Salaam chini ya kocha Kim
Poulsen.
Serengeti Boys inayofanya
mazoezi Uwanja wa Karume itahitimisha kambi hiyo Machi 9 mwaka huu kwa kucheza
mechi na timu ya U20 ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani ambayo iko Ligi Kuu ya
Vodacom.
Baada ya Serengeti Boys
kumaliza kambi Machi 9 mwaka huu, siku hiyo hiyo timu ya Taifa ya vijana wenye
umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) nayo itaingia kambini chini ya
Poulsen katika mpango wa timu hizo kufanya mazoezi ya wiki moja kila mwezi na
kucheza mechi moja.