Beki wa Sunderland Wayne Bridge (kushoto) akigombea mpira na kiungo wa Everton, Tim Cahill (kulia) |
BAO la Tim Cahill kipindi cha kwanza limeipeleka Everton katika
mechi ya marudiano ya Kombe la FA dhidi ya Sunderland baada ya timu hizo za
Ligi Kuu kutoka sare ya 1-1 kwenye Robo Fainali.
Phil Bardsley alifunga bao la kuongoza kwa Sunderland dakika
ya 12 kwenye Uwanja wa Goodison Park kwa shuti la mbali, lakini Cahill akasawazisha
dakika 11 baadaye.
Tottenham inaikaribisha Bolton baadaye katika mchezo
mwingine wa Kombe la FA wakati kwenye Ligi Kuu kuna mechi mbili kati ya Fulham
vs. Swansea na Wigan vs. West Bromwich Albion.