MABINGWA wa ligi kuu ya soka Tanzania bara msimu wa 2010/2011timu ya Yanga inadaiwa ipo katika mazungumza na kutaka kumsajili kiungo wa Simba, Rashid Gumbo, imefahamika.
Habari zilizopatikana jana kutoka Yanga zinasema kuwa Gumbo aliingua katika mazungumzo na kamati ya usajili chini ya mwenyekiti wake Seif Ahmed bada ya kuona Simba haina mpango wa kumsajili.
Kiungo huyo wa zamani wa timu za African Lyon na Mtibwa Sugar ya Morogoro ni miongioni mwa viuongo bora wenye uwezo wa kutoa pasi bora murua za mwisho, akiwa na uwezo pia wa kufunga kwa kupitia mipira iliyokufa ingawa tatizo lake huonekana hana msaada timu inapoelemewa.
Iwapo Yanga itafanikiwa kumsajili kiungo huyo itakuwa imesajili wachezaji wanne mpaka sasa baada ya kipa Said Mohammed (Majimaji ya Songea), Godfrey Taita (Kagera Sugar) na Pius Kisambale (JKT Ruvu).
Aidha, Yanga ipo katika mazungumzo na kiungo wa APR ya Rwanda, Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, mshambualiaji wa SK Jagodina ya Serbia, Kenneth Assamoh, kiungo wa Simba Mohammed Banka na kipa wa Mtibwa Sugar, Shaban Kado.