Na Ghisa Abby, Kilosa
WASANII mahiri
wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Selemani Msindi, ‘Afande Sele’ na Abbas
Kinzasa, ‘20%’ juzi walizua tafrani kubwa mjini Morogoro iliyowasababishia
kutupwa rumande baada ya kukosa dhamana mahakamani.
Imeelezwa kuwa
wasanii hao juzi, walifika na gari lao katika maeneo ya Benki ya NMB Tawi la
Wami, ambako katika kupaki kulitokea kutoelewana na askari wanaolinda usalama,
hivyo kuzuka kwa tafrani kubwa.
“Baada ya
kutokea mzozo huo, wananchi nao wakaanza kuingilia, hivyo kuzuka tafrani kubwa,
ikiwamo kuharibiwa kwa baadhi ya magari yaliyokuwapo eneo hilo na askari mmojawapo kuumizwa,” kilisema
chanzo hicho na kuongeza:
“Ilibidi askari
wafike na kutumia nguvu kuwatawanya wananchi, huku Afande Sele na 20% wakitiwa
mbaroni na kufikishwa mahakamani jana, ambako walikosa dhamana na kutupwa
rumande.”