TIMU ya
soka ya Young Muslim imeondoka jijini Dar es Salaam leo kuelekea Nairobi,
Kenya kushiriki mashindano ya Sunni Muslim Football Tournament yanayotarajiwa
kuanza kesho mjini humo.
Meneja wa timu hiyo Salim Issak alisema kuwa mashindano hayo
yanahusisha timu zilizopo chini ya Jumuiya Muslim Janat kutoka miji ya Dar es
Salaam, Arusha, Zanzibar na Mombasa.
Alisema
kuwa kikosi chake kimejiopanga vema kuhakikisha kinashinda michuano hiyo yenye
lengo la jumuiya hizo, inatarajiwa kumalizika Aprili 9.
Aliongeza
kuwa msafara wa watu 25 wakiwemo viongozi watano na wachezaji 20 umeondoka
chini ya udhamini wa Nitak, Muza Oil Mills, Arif Khatri na Kilombero Sugar.
Bingwa
mtetezi wa michuano hiyo ni timu ya Mombasa ambapo timu Young Muslim ilitwaa
kombe hilo kwa mara ya mwisho mwajka 2010 katika michuano iliyofanyika Visiwani
Zanzibar.