AL AHLY WAFANYA SIRI UJIO WAO, KUWASHUHUDIA KWA BUKU 5

WAPINZANI wa Simba katika kombe la CAF, Al Ahly Shandy ya Sudan mpaka sasa hawajatoa taarifa ya ujio wao nchini, imefahamika.
Timu hizi zinatarajiwa kukwaana Aprili 29 kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika mchezo wa awali ambapo uongozi wa Simba umesema hauna taarifa juu ya ujio wao.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' ameiambia mamapipiro blog kwamba pamoja na wapinzani hao kuficha juu ya ujio wake wameshatuma taarifa kuhusiana na mchezo huo kwa chama cha soka cha Sudan.
Amesema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea ambapo waamuzi na kamishna kutoka Swaziland wanatarajiwa kuwasili ijumaa.
Aidha, viiongilio vya mchezo huo ni shilingi 5,000 ni kwa kiingilio cha chini na cha juu shilingi 30,000 ambapo tiketi zitaanza kuuzwa ijumaa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

Previous Post Next Post