TENGA AKATAA KUJIUZULU KWA
MOHAMED
Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF) Leodegar Tenga amekataa barua ya kuomba kujiuzulu ya
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Said Mohamed.
Mohamed ambaye ni Mwenyekiti
wa klabu ya Azam alimuandikia Rais Tenga barua ya kujiuzulu wadhifa huo akipinga
kauli ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Alfred Tibaigana juu ya adhabu
zilizotolewa na Kamati ya Ligi kwa baadhi ya wachezaji wa Yanga.
Rais Tenga amesema alimteua
Mohamed katika Kamati hiyo kwa kuzingatia uadilifu wake na uwezo wake katika
kuongoza, hivyo amekataa barua hiyo ya kuomba kujiuzulu.
Kwa mujibu wa mamlaka
aliyopewa na Mkutano Mkuu wa TFF, Rais Tenga, Oktoba 28 mwaka jana aliunda
Kamati ya Ligi ambayo wajumbe wake wanatoka kwenye klabu za Ligi Kuu ya Vodacom
na Ligi Daraja la Kwanza.
Wajumbe wa kamati hiyo ni
Wallace Karia (Mwenyekiti), Said Mohamed (Makamu Mwenyekiti), Damas Ndumbaro,
Steven Mnguto, Geoffrey Nyange, Seif Ahmed, Henry Kabera, ACP Ahmed Msangi, Meja
Charles Mbuge na Ahmed Yahya.
WASHABIKI 11,056 WASHUHUDIA
COASTAL, YANGA
Washabiki 11,056 ndiyo
waliokata tiketi kushuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Coastal
Union na Yanga lililochezwa juzi (Machi 31 mwaka huu) kwenye Uwanja wa
Mkwakwani, jijini Tanga.
Viingilio katika pambano hilo
vilikuwa sh. 10,000 kwa VIP, sh. 6,000 jukwaa kuu na sh. 4,000 mzunguko. Mapato
yaliyopatikana kwenye pambano hilo ni sh. 61,494,000.
Baada ya kuondoa gharama za
awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu
ilipata sh. 14,664,927.80 uwanja sh. 4,630,335.93 na Chama cha Mpira wa Miguu
Mkoa wa Tanga (DRFA) sh. 2,515,494.37.
Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) sh. 4,630,335.93, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
2,315,167.97 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh. 463,033.59.
Nayo mechi kati ya African
Lyon na Simba iliyochezwa Machi 31 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam imeingiza sh. 29,716,000 kutokana na watazamaji 8,167 waliokata tiketi
kushuhudia pambano hilo.
Baada ya kuondoa asilimia 18
ya VAT ambayo ni sh. 4,532,949.15, kila timu ilipata sh. 5,031,085.25, Uwanja
sh. 1,486,465.08, TFF sh. 1,486,465.08, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 1,084,600.03, FDF sh. 743,232.54 na BMT sh.
148,646.51.
AZAM, RUVU STARS ZAINGIZA MIL
1.5
Pambano la Ligi Kuu ya
Vodacom kati ya Azam na Ruvu Stars lililochezwa jana (Aprili Mosi mwaka huu)
Uwanja wa Chamazi, Dar es Salaam limeingiza sh. 1,585,000.
Jumla ya watazamaji waliokata
tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 1,000 mzunguko na sh. 5,000
jukwaa kuu ni 1,569.
Baada ya kuondoa gharama za
awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kila timu
ilipata sh. 283,656, uwanja sh. 57,942, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es
Salaam (DRFA) sh. 117,306.08, TFF sh. 57,942, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa
Miguu (FDF) sh. 28,971 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) sh.
5,794.02.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Kwani hili bango halina maelezo, mbona mmetuwekea frem tupu ?
ReplyDelete