Van Persie na Theo |
MSHAMBULIAJI Robin van Persie amejisikia vibaya baada ya
kipigo cha Jumamosi kutoka kwa Queens Park Rangers, lakini amesema makali ya
Arsenal yatarejea watakapokwenda kucheza na Manchester City.
Mholanzi huyo alishuhudia rekodi ya timu yake kushinda mechi
saba mfululizo ikizimwa kwenye Uwanja wa Loftus Road, shukrani kwao Adel
Taarabt na Samba Diakite kwa mabao yao siku hiyo.
Arsenal inabaki nafasi ya tatu, lakini inalingana kwa pointi
na Tottenham, ambayo iliifunga Swansea City 3-1 jana.
"Kila mmoja amesikitishwa, lakini kuelekea mwishoni mwa
wiki nina uhakika kwamba makali yatakuw akama yalivyokuwa," alisema Van Persie.
"Tutakuwa na siku kadhaa za masikitiko, lakini baada ya hapo, fikra zetu
ni kwa Manchester City.
Dada wewe ni mwandishi wa habari, unapochukua habari hii bila kuquote umeiota wapi ni kosa...walau tupeni na sisi heshima...
ReplyDelete