MWIMBAJI na Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ali Choki alisema
kwamba kwa sasa amejikuta akichukiwa na Mkurugenzi wa African Stars ‘Twanga
Pepeta’, Asha Baraka kwa madai ya kuhamisha wanamuziki wake na kuwaajiri.
Choki aliyasema hayo wakati alipokuwa akifanya mahojiano na
televisheni moja maarufu ya jijini hapa ambako alisema anashangaa kumuona
mkurugenzi wake wa zamani Asha Baraka
akimchukia wakati anajua waimbaji wanahama kwa ajili ya kutafuta
maslahi.
“Kuhama kwa waimbaji ni kujitafutia maslahi lakini
nashangaa kwa nini Mkurugenzi mwenzangu wa Tweanga anachukia hilo . Si kwangu bali kwa bendi nyingi tu,”
alisema.