Diamond akipongezwa |
Khadija kopa |
Roma katikati, kulia Profesa Jay na kushoto said Fela |
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe akimpa tuzo Diamond |
MSANII Nassib Abdul ‘Diamond’
usiku huu ameng’ara kwenye tuzo za Kilimanjaro Music Award, baada ya
kujinyakulia tuzo tatu.
“Namshukuru Mungu, wakati
mwingine uvumilivu na subira ni mzuri. Mwaka jana sikupata tuzo, nikamshukuru
Mungu, nikaongeza bidii, nikafanya kazi nzuri, leo ninachukua tuzo ya tatu sasa
hivi, alisema Diamond kuambia bongostaz baada ya kushinda tuzo ya Video Bora ya
Mwaka, kupitia wimbo Moyo Wangu, ambayo ilikuwa ya tatu usiku huu.
Diamond alizishinda nyimbo za Hakunaga
ya Suma Lee, Wangu ya Jay Dee, Ndoa Ndoana ya Kassim na Bongo Fleva ya Dully Sykes.
Barnaba aliibuka Mwimbaji Bora
wa Kiume, akiwashinda, Ally Kiba, Diamond, Belle 9 na Mzee Yussuph.
Tuzo ya waliochangia mafanikio
ya muda mrefu ilikwenda kwa JKT Taarab, marehemu Dk Remmy Ongala na King Kiki.
Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jaydee’
alishinda tuzo ya Mwimbaji Bora wa Kike, akiwashinda Linah, Khadija Kopa, Dayna
na Isha Mashauzi.
Ommy Dimpoz aliwabwaga Darasa, Rachel,
Abdul Kiba na Beatrice aka Nabisha katika tuzo ya Msanii Anayechipukia.
Ommy Dimpoz alimpa nafasi Diamond
kuelezea namna prodyuza mmoja alivyomkatisha tamaa wakati anaanza muziki.
“Nilimpeleka Ommy kwa prodyuza
wangu, nikamuambia msaidie huyu kijana, anaweza naye ainuke kama sisi, lakini yule
prodyuza akasema dogo hawezi kuimba. Ila wimbo ule ule, amerekodi na leo unampa
tuzo,”alisema Diamond.
Katika wimbo bora wa mwaka,
mshindi alikuwa ni Suma Lee kupitia wimbo wake Hakunaga, akiwashinda Ally Kiba
na Dushelele, Diamond na Moyo Wangu, Roma na Mathematics, Nilipe Nisepe wa
Belle 9 na Riz One wa Izzo B.
Bahati mbaya Suma Lee hakuwepo
na tuzo zake alichukuliwa na Babu Tale.
Katika wimbo bora wa Zouk
Rhumba, Ally Kiba, kupitia wimbo wake Dushelele aliwabwaga Barnaba na wimbo
wake Daima Milele, Dayna na Nivute Kwako Lady Jaydee, aliyemshirikisha Mr Blue
katika Wangu na Kizunguzungu wa Rachel.
Diamond alibeba tuzo ya Mtunzi Bora wa Mwaka, akiwaangusha Ally Kiba, Mzee Yussuph,
Barnaba na Belle 9, wakati wimbo bora wa kushirikiana, Ommy Dimpoz na Ally Kiba
waling’ara kupitia kibao chao Nai Nai, Famous wa Jay Mo na P Funk, King Zilla wa
Godzilla na Marco Chali na Wangu wa Jay Dee na Mr. Blue na Kama ni Gangstar wa Chege,
Mh Temba na Ferooz.
Katika wimno bora wa Raggae,
kibao cha Arusha Gold cha Warriors From East kiling’ara mbele ya Mazingira wa
Malfred aliyemshirikisha Lutan Fyah, Give It Up To Me wa Delyla Princess, Nia Yao
wa 20% na Ni Wewe wa Nakaaya.
Katika wimbo bora wa Ragga,
Dancehall, Maneno Maneno wa Queen Darleen, ulizishinda Good Look wa AY
aliyemshirikisha Miss Trinity, Ganja Man wa Dabo, Kudadeki na Poyoyo za Malfred.
Katika wimbo bora wa Taarab,
Isha Mashauzi kupitia wimbo wake Nani Kama Mama uliushinda wimbo wake Mama
Mashauzi, Full Stop wa Khadija Kopa, Hakuna Mkamilifu na Nilijua Mtasema za
Jahazi.
Katika wimbo bora wa Kiswahili wa
bendi, African Stars ‘Twanga Pepeta’ liling’ara kupitia wimbo wa Dunia Daraja
ikizishinda Mashujaa na
Hukumu ya Mnafiki na Mtenda za
Extra Bongo na Falsafa ya Mapenzi, Mapacha Watatu na Usia wa Babu.
Rapa bora wa bendi wa mwaka
alikuwa ni Kalidjo Kitokololo wa FM Academia, aliyewashinda Khalid Chokoraa, Feguson,
Msafiri Diouf na Totoo ze Bingwa.
Msafiri Diouf alipanda jukwaani
na kukiri kushindwa- akimwagia sifa Kitokololo kwamba alistahili.
Katika wimbo bora wa Afri Pop,
Suma Lee aliibuka mshindi kutokana na kibao chake Hakunaga, kilichozishinda Bongo
Fleva wa Dully Sykes, Moyo Wangu na Mawazo za Diamond na Nai Nai wa Ommy Dimpoz.
Katika Mtumbuizaji Bora wa
Kiume, Diamond aliwaangusha Ally Kiba, Dully Sykes, Bob Junior na Mzee Yusuph,
wakati Mtumbuizaji Bora wa Kike, Khadija Kopa aliwaangusha Isha Mashauzi, Queen
Darleen, Dayna na Shaa.
Katika wimbo bora wa R&B,
Ben Pol kupitia kibao chake My Number Fun, kiliushinda wimbo wake Maumivu, Nilipe
Nisepe wa Belle 9, Usiniache wa Hemed na Napata Raha wa Jux.
Roma aliibuka kidedea katika
wimbo bora wa Hip hop, kupitia wimbo wake Mathematics, uliozishinda Famous, King
Zilla, Riz One na Kilimanjaro.
Roma aling’ara pia katika tuzo
ya Msanii Bora wa Hip Hop, akiwashinda Godzilla, Izzo B, Joh Makini na Fid Q.
Baada ya kuchukua tuzo hiyo pia,
Roma aliwaambia wasanii wengine wa Hip hop kwamba anastahili.
Jaguar wa Kenya alishinda tuzo
ya wimbo bora wa Afrika Mashariki, kupitia wimbo wake Kigeugeu, uliozishinda Chokoza,
Mulika Mwizi, Coming Home na 4 Sho 4 Shizzle.
Maneka wa AM Records alishinda
tuzo ya Mtayarishaji Bora wa Nyimbo, akiwaangusha Marco Chali, Pancho Latino, Bob
Junior na Man Walter.
BURUDANI ILIPOOZA:
Sambamba na utoaji wa tuzo,
kulikuwa na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali- lakini kwa ujumla
sekta hiyo mwaka huu ilidorora.
Si kwa sababu ya wasanii wa
Tanzania pekee kutumbuiza, la hasha- bali watumbuizaji wenyewe walishindwa
kusisimua watu.
Angalau kidogo Khadija Kopa
aliwarusha watu, lakini wengine walipitisha ratiba tu.
it was good kwa kweli congrats kwa wote walioshinda.......
ReplyDeleteIT WAS GOOD,VIJANA WALISTAHILI
ReplyDelete