JOTO la mchezo wa marudainoa wa kombe la Shirikisho (CAF) baina ya Simba na Es Setif ya Algeria limezidi kupanda baada ya wachezaji wa ES Setif kutishia kugoma wakishinikiza walipwe posho zao.
Taarifa za mtandao wa klabu hiyo zimeeleza kuwa tangu juzi mchana wachezaji hao kupitia kwa walitoa taarifa kwa uongozi kuhusiana na mgomo huo wakitaka kulipwa fedha hizo.
Imeelezwa kuwa kipindi timu hiyo ilipokuwa chini ya umiliki wa Setif haikuwa na matatizo lakini tangu iwe chini ya wafadhili mambo yameonekana kwenda mrama.
Hatua hiyo ni kicheko kwa Simba ambayo itatuamia vema mapungufu hayo kuhakikisha inashinda na ugenini na hatimaye kusonga mbele katika michuano hiyo.
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki nchini wiki iliyopita Simba ilishinda mabao 2-0.