KLABU ya Manchester United iko katika majonzi kufuatia kifo
cha Mkurugenzi wake wa zamani, Amer Midani.
Mzaliwa huyo wa Beirut mwaka 1957, Mr Midani alijiunga na
klabu hiyo ya Old Trafford mwaka 1987 wakati United ilipoinunua klabu ya mpira
wa kikapu ya Manchester Giants, ambayo alikuwa Mwenyekiti
wake.
Awali alikuwa raia wa Lebanon na bingwa wa michuano ya watoto
ya table tennis akiwa ana umri wa miaka 15 na alihamia England akiwa ana umri wa
miaka 18.