Kocha Kim Poulsen, leo
(Aprili 10 mwaka huu) ametaja kikosi cha wachezaji 21 wa timu ya Taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya mechi ya michuano
ya Afrika kwa umri huo.
Kikosi hicho kimeingia
kambini leo (Aprili 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi dhidi
ya Sudan itakayochezwa Aprili 21 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa.
Wachezaji walioitwa kwenye
kikosi hicho ni Saleh Ally Malande (Simba), Aishi Salum Manula (Azam), Hassan
Khamis Kessy (Mtibwa Sugar), Said Ruhava Samir (Falcon, Pemba), Carlos Protus
Kilenge (TSC Mwanza), Dizzana Issa Yarouk (Azam), Amani Peter Kyata (African
Lyon) na Issa Rashid Issa (Mtibwa Sugar).
Emily Mgeta Josiah (TSC
Mwanza), Khamis Jamal Mroki (Mtibwa Sugar), Ramadhan Suzana Singano (Simba),
Frank James Sekule (Simba), Frank Domayo Raymond (JKT Ruvu), Omega Sunday Seme
(Yanga), Abdallah Kilala Hussein (Falcon, Pemba) na Ibrahim Rajab Juma (Villa
Squad).
Hassan Saleh Dilunga (Ruvu
Shooting), Alhaje Said Zege (JKT Ruvu), Jerome Lambele Reuben (Moro United),
Atupele Green Jackson (Yanga), Simon Msuvan Happygod (Moro United) na Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo).
Mechi ya marudiano dhidi ya
Sudan itachezwa jijini Khartoum kati ya Mei 4, 5 na 6 mwaka huu.
Fainali za Afrika kwa vijana zitafanyika
Machi mwakani nchini Algeria. Timu nne za juu kwenye fainali hizo zitacheza
Fainali za Dunia zitakazofanyika nchini Uturuki kuanzia Juni hadi Julai mwaka
huu.