SIMBA, SIMBA, SIMBA...RAHA TUPUUU


Mashabiki wa Simba 

WEKUNDU wa Msimbazi, Simba SC jioni hii wamejihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kuifunga Moro United ya Morogoro maba 3-0 na mechi ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa,  Azam FC dhidi ya Mtibwa Sugar ikivunjika timu hizo zikiwa zimefungana 1-1, Uwanja wa Azam, Chamazi.
Mabao ya Simba SC yalifungwa na Patrick Mutesa Mafisango, Haruna Moshi Shaaban 'Boban' na Felix Mumba Sunzu Jr.
Simba sasa imetimiza pointi 59, ambazo kutokana na matokeo ya leo ya sare ya 1-1 kati ya azam na Mtibwa, haziwezi kufikiwa na timu yoyote. Lakini kujiweka salama, Simba itahitaji japo polnti moja katika mechi zake tatu zilizobaki. 
Mchezo kati ya Azam na Mtibwa ulivunjika wakati beki Salum Swedi amekwishaifungia bao Mtibwa na Mrisho Khalfan Ngassa ameifungia Azam FC. Mtibwa waligomea mechi hiyo wakipinga Azam kupewa penalti. Sasa Kamati ya Ligi Kuu itakutana kesho na kutoa uamuzi, lakini kuna uwezekano mkubwa Mtibwa ikatozwa faini na wapinzani wao kupewa ushindi.

Post a Comment

Previous Post Next Post