WAWAKILISHI pekee wa Tanzania kwenye kombe la Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Simba wamewaomba mashabiki wa timu mahasimu wao Yanga kujitokeza kwa wingi katika dimba la Taifa jumapili ya keshokutwa kuwashangilia wapakapokwaana na Al Ahli Shandy ya Sudan.
Simba na wasudan hao watacheza m,chezo wao wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya michuano ya CAF ambapo tayari Al Ahli wametua nchini tangu jana.
Makamu Mwenyeketi wa Simba Geofrey Nyange 'Kaburu' ameiambia mamapipiro blog kwamba kikosi cha Simba kipo katika hali nzuri na kinaendelea na mazoezi yake ya kawaida.
Alisema ili kuipa sapoti timu hiyo iweze kuccheza kwa nguvu zote amewaomba mashabiki wote wa soka nchini wakiwemo wa Yanga kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya jumapili.
Kila la kheri Simba hiyo jumapili, nadhani mmejiandaa vya kutosha kukabiliana na hao wasudan.Ushindi mkubwa ndio silaha hawa ni waarabu wana mizengwe kweli kweli ukienda kwao.
ReplyDeleteHeshima kwako dada Dina Ismail kwa kutupasha habari.