CHAMA
cha Soka Zanzibar (ZFA), leo kinatarajia kusaini mkataba wa udhamini wa Ligi
Kuu ya Zanzibar
na kampuni inayotengeneza kinywaji cha Grand Malt.
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari wa ZFA, Munir Zakaria, utiaji saini mkataba huo wa miaka
mitatu, ni faraja kubwa kwa klabu 12 za ligi hiyo baada ya kujiondoa kwa Kampuni ya
Usafirishaji wa Baharini ya Seagull mapema mwaka uliopita kutokana na sababu za
kiuendeshaji.
Munir,
alisema, ZFA ikiwa ndiyo mlezi wa klabu za soka, imefarijika kutokana na
kujitokeza kwa mdhamini huyo ambaye ameahidi kurudisha ushindani wa ligi hiyo
masikini visiwani hapa.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyosambazwa kwa vyombo vya habari, Grand Malt itadhamini
ligi ya msimu ujao utakaoanza Agosti kwa thamani ya shilingi milioni 140.
Munir
alisema, klabu zinatarajiwa kupatiwa kiasi cha shilingi milioni nane kila moja zikiwemo
fedha za usafiri pamoja na mahitaji mengine ya kujikimu kwa ajili ya vyakula na
malazi wakati zitakapokuwa kwenye vituo Unguja na Pemba