Simba SC |
SIMBA SC imefuzu kuingia Raundi ya
Tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka CAF, kwa faida ya bao la ugenini baada ya
kufungwa mabao 3-1 na ES Setif kwenye Uwanja wa Mei 8, mjini Setif katika
mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Shukrani kwake mshambuliaji wa
kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi aliyefunga bao la dakika za lala salama
wakati refa amekwishaonyesha dakika za majeruhi tano.
Katika mchezo huo, Simba ilipata
pigo mapema dakika ya 18 baada ya beki wake Juma Said Nyosso kutolewa nje kwa
kadi nyekundu kwa kucheza ‘rafu ya wazi’.
Hadi mapumziko, tayari Setif
walikuwa mbele kwa mabao 2-0 na mapema kipindi cha pili, wakapiga la tatu.
Mchezo wa kwanza Simba ilishinda
2-0 Dar es Salaam na sasa itamenyana na Al Ahly ya Sudan.
Simba wacheka kama kibelala.....mhhhh......aaaahhh.......mhhhh......aaaahhh,weekend yetu itakuajema eee,simbaaaaaaa!
ReplyDeleteBIG UP SSC
ReplyDelete