SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu Tanzania(TBF) limewafungulia wachezaji wa timu hiyo na kubakiza adhabu kwa viongozi.
Rais wa TBF Musa Mziya
alisema kuwa wameawafungulia wachezaji hao baada ya kuandika barua
ya kukiri kosa na kudai kuwa lilisababishwa
na viongozi walioambatana na timu kuwashawishi wachezaji kuvunja kanuni za
mashindano.
Alisema kuwa pamoja na kuondoa adhabu hiyo TBF imewataka wachezaji hao kulipa faini ya sh 300,000 kabla ya kuanza kushiriki
shughuli zozote za mpira wa kikapu.
“kamati ya utendaji inautaka mkoa wa mwanza kuendelea
kujitafakari katika nidhamu na uvunjaji wa amani ya mchezo,na TBF itakuwa
inasimamia na kuhusika kwa kipindi cha mwaka mmoja wa adhabu kwa kaimu
mwenyekiti MRBA Kizito Bahati,Robert Mwita ambaye ni kocha na kocha msaidizi
Amri Mohamed”alisema Mziya