Kikao cha
Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kilichokuwa
kifanyike kesho (Aprili 14 mwaka huu) kujadili rufani ya Yanga kupinga
kunyang’anywa pointi tatu kwa kumchezesha Nadir Haroub katika mechi dhidi ya
Coastal Union kimeahirishwa.
Kamati hiyo
chini ya uenyekiti wa Kamishna mstaafu wa Polisi, Alfred Tibaigana sasa
kitafanyika Jumanne (Aprili 17 mwaka huu) saa 9 alasiri kwenye ofisi za TFF.
MIKOA 13
YAWASILISHA MABINGWA WAKE
Vyama vya
mpira wa miguu vya mikoa 17 ya Tanzania Bara vimewasilisha majina ya mabingwa
wake kwa ajili ya Ligi ya Taifa iliyopangwa kuanza Aprili 22 mwaka huu katika
vituo vitatu.
Mikoa hiyo
na mabingwa wake katika mabano ni Kigoma (Kanembwa FC ya Kibondo), Kilimanjaro
(Forest FC ya Siha), Ruvuma (Mighty Elephant ya Songea), Dodoma (CDA), Rukwa,
(Mpanda Star ya Mpanda), Iringa (Kurugenzi FC ya Mufindi) na Lindi (Lindi SC ).
Mingine ni
Mtwara (Ndanda FC), Shinyanga (Mwadui FC), Mara (Polisi Mara), Singida (Aston
Villa), Arusha (Flamingo SC) na Tabora (Majimaji FC). Mikoa ambayo
haijawasilisha mabingwa wake ni Manyara, Dar es Salaam, Mwanza, Tanga,
Morogoro, Pwani na Kagera.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF)