MWILI wa mjumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu ya Yanga Theonest Rutashoborwa (pichani)unatarajiwa kuagwa jumatatu ijayo katika kanisa katoliki parokia ya kijichi kabla ya kusafirishwa kwenda kwao kijiji cha Bukabaye kilicopo Bukoba mkoani Kagera.
Rutashoborwa
ambaye kitaaluma ni wakili akimiliki kampuni ya Brilliance Law Chambers ya
jijini Dar es Salaam alikutwa na umauti huo usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Agha Khan
alipokwenda baaada ya kujisikia vibaya kabla ya kubainika kuwa na kisukari na shinikizo la damu.
Ofisa habari wa yanga, Louis Sendeu
amesema kuwa Rutashoborwa alianza kujisikia vibaya mara alipotua uwanja wa ndege wa
mwalimu Jk Nyerere akitokea Moshi, Kilimanjaro alipokwenda kwa shughuli zake za
kikazi na alipokimbizwa hoispitalini alifariki akiwa katika harakati za
kupelekwa chumba cha uangalizi maalum (ICU).
“Yanga
inasikitisha kumpoteza kiongozi huyu hidari ambaye alikuwa muhimili mkuu katika
kuinganisha Yanga, kwa nianba ya wanachama na wapenzi wa Yanga tunatoa pole kwa
familia ya marehemu, ndugu jamaa na marafiki,”Alisema Sendeu.
“Marehemu
ameacha mjane na watoto wanne, bwana ametoa Bwana ametwaa, mwenyezi mungu
aiweke rioho ya marehemu mahali pema peponi, Amin,”Alisema.