WAKATI
kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka Tanzania (TFF) ikitarajiwa kukutana kesho kwa
ajili ya kujadili rufaa ya klabu ya Yanga kupokwa pointi, klabu ya Yanga
imeitaka kamati hiyo kutoa maamuzi ya haki.
Ofisa
habari wa Yanga Louis Sendeu (pichani)amesema kwamba wameamua kutoa hadhari hiyo
kutokana na utata uliopo katika suala hilo
kwani wengi wameshindwa kuelewa sababu iliyopelekea Yanga kukata rufaa.
Alisema wamekata
rufaa kupinga kupokwa pointi taru na mabao matatu na kamati ya ligi kutokana na
kumchezesha beki wao Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ambaye alikuwa anatumikia adhabu
ya kadi nyekundu alipopewa wakati Yanga ikicheza na Azam Fc ambapo kulitokea
vurugu.
“Maamuzi
yalisema Cannavaro alipewa kadi nyekundu kwa utovu wa nidhamu na si kumpiga
mwamuzi...kikanuni anapaswa kukosa mechi mbili na ndivyo ilivyokuwa, lakini kama angepaswa kukosa mechi tatu tungeandikiwa barua,”Alisema.
Sendeu
aliongeza kuwa iwapo hawatarejeshewa pointi hizo walizopewa Coastal Union
watakata rufaa kwenye kamati ya Rufaa ya TFF.
Kamati hiyo
nidhamu chini ya mwenyekiti wake Kamisha mstaafu wa polisi,Alfred Tibaigana
itapitia na kutoa maamuzi ya rufaa hiyo ya Yanga ambayo kamati ya Ligi TFF
iliipa Coastal Union ushindi kwa kuzingatia kanuni ya 25(f) ya Ligi Kuu ya
Vodacom juu ya Udhibiti wa Wachezaji inayosema: “Ni lazima kwa klabu na
wachezaji kutunza kumbukumbu za kadi. Klabu itakayomchezesha mchezaji mwenye
kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu itapoteza mchezo na timu pinzani
itapewa ushindi wa pointi tatu (3) na mabao matatu (3), iwapo mchezaji atacheza
akiwa haruhusiwi kucheza kwa ajili ya kadi tatu (3) za njano au kadi nyekundu
timu yake itapoteza mchezo. Endapo klabu haina uhakika au inataka taarifa ya
idadi ya kadi zake itaomba kwa maandishi toka TFF.”
Kwa mujibu
wa kamati ya Ligi, Cannavaro alioneshwa kadi nyekundu kwa kosa la kupigana
kwenye mechi kati ya Yanga na Azam iliyochezwa Machi 10 mwaka huu ambapo kwa
mujibu wa Kanuni ya 25(c) ya Ligi hiyo anastahili kukosa mechi tatu lakini
alikosa mechi mbili tu.