TWanga Pepeta
Isha Mashauzi
Na Mwandishi Wetu
Bendi za African
Stars “Twanga Pepeta” na Mashauzi Classic “Wakali wa Kujiachia” watatumbuiiza
kwenye onyesho la utambulisho wa Miss Tabata 2012 siku ya Pasata katika ukumbi
wa Dar Wes Park, Tabata.
Mratibu wa
shindano hilo Godfrey Kalinga alisema jana kuwa bendi hizo mbili zitafanya
maonyesho yao kabla ya warembo kutambulishwa na hata baada ya utambulisho
zitaendelea kutoa burudani kali hadi majogo huku wapenzi wao wakisherekea sikuku
ya Pasaka.
Kalinga alisema
onyesho hilo maalum imeandaliwa na Bpb Entertainment na Keen Arts chini ya
udhamini wa Konyagi.
Pia alisema
itakuwa ni onyesho maalum ya kusherekea sikukuu ya Pasaka na kutambulisha
warembo watakaoshiriki kwenye shindano la kumsaka Miss Tabata 2012 ambalo
limepangwa kufanyika mwezi ujao.
“Wapenzi wa
muziki na urembo siku hiyo watapata fursa ya kuwaona warembo hao kabla ya
kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata ambalo limepangwa kufanyika mwishoni
mwa Mei,” alisema Kalinga.
Mratibu huyo
alisema warembo wanaotaka kushiriki kwenye shindano la Miss Tabata wanaendelea
na mazoezi katika ukumbi wa Dar West Park, Tabata chini ya wakufunzi watatu -
Beatrice Joseph, Neema Chaki na Bokilo Junior.
Warembo hao
ni Neema Saleh (18), Paulina Valentine (18), Khadija Nurdin
(19), Phillos Lemi (20) na Mercy Mlay (21).
Wengine ni
Neema Innocent (19), Ellen Sule (22), Wikllihemina
Mvungi (20), Queen Issa (20), Suzane Deodatus (19), Everline Andrew (21),
Josephine Peter (20) na Jamila Omary (19). Warembo hao wako
Zaidi ya warembo
10 kutoka Tabata watafuzu kushiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala,
Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Mrembo
anayeshikilia taji la Tabata ni Faiza Ally.
Warembo wa Tabata wamekuwa wakifanya vizuri
katika mashindano ya Miss Tanzania ambapo mwaka juzi Consolata Lukosi alishinda
nafasi ya tatu kabla ya kutangazwa kuwa balozi wa kinywaji cha Redds. Katika
shindano la mwaka juzi Julliet William pia alishinda nafasi ya tatu katika ngazi
hiyo ya taifa.