TIMU za vijana wenye umri
chini ya miaka 20 za Azam Fc na Simba keshokutwa zinatarajiwa kukwaana katika dimba
la Chamazi ikiwa ni mchezo maalum wa kuadhimisha kifo cha rais wa kwanza wa Zanzibar , Abeid Aman
Karume.
Msemaji msaidizi wa Azam Fc Jaffer Idd Maganga alisema maandalizi kwa ajili ya
mchezo huo yanakwenda vizuri.
Alisema timu hizo ambazo
zimekuwa zikichuana vikali katika michuano mbalimbali ya Vijiana ikiwemo ile
inayoshirikisha timu za Vijana ‘Uhai Cup’
ambapo Simba inashikilia ubingwa.