WASANI WAPIGANA VIKUMBO KUNUNUA NGUO, VIATU, KUKODI MAGARI YA KIFAHARI KWA AJILI YA KUHUDSHURIA MAZISHI YA KANUMBA



WAKATI leo safari ya mwisho ya msanii wa filamu nchini ikitarajiwa kuhitimishwa leo, kuna habari kuwa kuna baadhi ya wasanii wenzake wamekuwa wakihaha tangu juzi katika maduka ya nguo na vipodozi kwa ajili ya kutafuta mavazi na nywele watakazovalia katika mazishi ya msanii huyo.
Pia kuna wengine wamekuwa wakihaha kusaka magari ya kifahari watakayokodi kwa ajili ya kuyatumia katika mazishi hayo.
KAnumba ambaye alikutwa na umauti usiku wa kuamkia Jumamosi nyumbani kwake Sinza anatarajiwa kuzikwa jioni ya leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo tayari maelfu ya watu wamefurika katika viwanja vya Leaders Kinondoni kwa ajili ya kuaga mwili wake.
Habari zinasema kuwa wasanii hao wameamua kutafuta nguo, viatu na vipodozi ili waweeze kuonekana nadhifu zaidi katika msiba huo uliogusa hisia za Taifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post