MAMBO ndani ya klabu ya Yanga yameendelea kuwa kizungumkuti baada
ya baadhi ya wanachama kumtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga ang'atuke
madarakani, kuwa ndiye chanzo cha timu hiyo kufanya katika mechi zake za Ligi
Kuu soka Tanzania Tanzania Bara.
Hatua hiyo inafuatia timu hiyo kupoteza mwelekeo katika
mechi zake za Ligi hiyo katika siku za hivi karibuni ambapo ilipokea vipigo viwili mfululizo na
hivyo kujikuta wakipoteza matumaini ya
kuwania hata nafasi ya pili ambayo itawawezesha kushiriki michuano ya kimataifa
mwakani.
Baadhi ya wanachama wallisema wameiambia mamapipiro blog
kwamba Nchunga na kamati nzima ya utendaji ya klabu hiyo haina budi kujiuzulu
ili kuepuka dhalili katika siku za baadaye.
“Hakuna haja ya kulitupia lawama benchi la Ufundi kwani Mwenyekiti ndiye aliyeliteua hivyo ni
yeye anatakiwa awajibike na si viongozi wa benchi la ufundi”, Alisema mmoja ya
wanacha aliyejitamnbulisha kwa jina la Ismail Shaban.
Aidha, Ismail ambaye ni mwanachama wa Tawi la kariakoo akiwa
ni Makamu Mwenyekiti wa kundi la ushangiliaji la Yanga Sapoti.alisema kuwa
Nchunga alipaswa kuwajibika tangu timu ilipopokwa pointi tatu na mabao matatu
na kamati ya ligi ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) na kupewa Coastal Union ya Tanga.
Alisema kama angekuwa kiongozi makini asingeruhusu beki wao
Nadir Haroub 'Cannavaro' acheze na matokeo yake baada ya kuona mambo yanakwenda
vibaya ameamua kuwatoa kafara wengine.
"Nasema hivi tutaendelea kumkumbuka sana Makamu wetu
Davis Mosha, kwa kuwa msimu uliopita tulishapoteza mwelekeo lakini kwa jitihada
za Mosha tuliweza kutwaa ubinghwa katiukja hali ambayo haikutarajiwa.
Mwanachama mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Abdul Nassoro (kadi namba 230), alisema kuwa Nchunga
anatakiwa awe wa kwanza kung'atuka kwani
yeye ndiye aliyeifikisha Yanga hapa ilipo.
"Hata wachezaji wenyewe hawana nidhamu na viongozi
wamekuwa mstari wa mbele kubariki madudu ya wachezaji na kuwatetea pale
wanapokosea, kama baba hana nidhamu lazima na mtoto atafuata tabia ya baba…Nchunga
aondoke kwa hiari yake yeye pamoja kamati zake alizounda kwani wameshindwa
kuinusuru timu ," alisema Abdul.
Naye Mwanachama Mohamed Bakari wa Yanga Bomba, alimtaka
Nchunga kuitisha mkutano wa dharura ili uongozi uweze kujibu maswali kutoka kwa
wanachama wake.
Aidha Mwanachama mwingine wa Yanga Hussein Makabuleta naye aliutaka uongozi wa Yanga kujiondoa madarakani ili kuachia wengine kuongoza klabu hiyo kwa lengo la kuiletea mafaniki.
hao wanachama waache uhuni,huyo mohammmed bakari sijui ndio nani,sisi kama bomba hatumjui mtu mwenye jina hilo,hivi uongozi huu ambao umetwa ubingwa wa africa mashariki na kati na vikombe vingine kibao uhukumiwe kwa kukosa ubingwa mwaka huu tu na tena timu bado ikiwa nafasi ya tatu au wana lao jambo hao wahuni...nchunga atabaki kuwa kiongozi mwenye mafanikio zaidi kwa miaka hii karibuni,kwani kaipa yanga ubingwa kwenye michuano ya kimataifa
ReplyDeletemdau wa bomba,revere,massachessetts