ASPIRE KUANZA KUSAKA VIPAJI MEI 21

Mchakato wa kusaka vipaji kwa chipukizi wenye umri chini ya miaka 14 kupitia mpango wa kukuza vipaji wa Aspire Football Dream ambao uko chini ya Idara ya Ufundi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utafanyika kuanzia Mei 21 mwaka huu. Vituo vitakavyohusika ambavyo kila kimoja kinatakiwa kuwa na watoto wasiopungua 176 na tarahe ya kufanyika mchakato huo kwenye mabano chini mng’amua vipaji (scout) kutoka Hispania ni Morogoro (Mei 21 mwaka huu saa 3 asubuhi) na Bagamoyo mkoani Pwani (Mei 21 mwaka huu saa 8 mchana). Vingine ni Kawe, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 3 asubuhi), Makongo, Dar es Salaam (Mei 22 mwaka huu saa 8 mchana) na Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam (Mei 26 mwaka huu saa 9 mchana). Mpango wa Aspire Football Dream unafadhiliwa na Mtoto wa Mfalme wa Qatar katika nchi 16 duniani kwa Tanzania una jumla ya vituo 14. Vituo vingine ni Kigamboni, Tandika, Ukonga, Kitunda, Mbagala, Magomeni na Tabata. Watoto watakaochaguliwa katika mchakato huo watakwenda katika mchakato mwingine kwa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Nairobi, Kenya. Watakaofuzu kutoka hapo ndiyo watakaokwenda kwenye vituo vya kuendeleza vipaji (centre of excellence) vya Aspire Football Dreams. Aspire ina vituo viwili vya kuendeleza vipaji ambavyo viko Doha, Qatar na Dakar, Senegal.

Post a Comment

Previous Post Next Post