MWANAMUZIKI wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa, Saulo
John ‘Ferguson’. aliyekuwa mapumzikoni nchini Afrika Kusini anatarajiwa kurejea nchini kesho asubuhi na usiku ataanza kufanya
vitu vyake kwenye ukumbi wa San Siro.
Meneja wa hiyo King Dodoo la
Buche, alisema kuwa mwanamuziki huyo aliyekuwa mapumzikoni nchini humo anarejea
na kuanza kazi yake kesho ambapo anatarajiwa kurudi na vitu
vipya kutoka nchini huko
Alisema katika onesho hilo Furguson atatumia nafasi hiyo
kuwaonjesha vionjo vypya alivyotunga akiwa nchini humo.
Naye Furguson ambaye alizungumza kwa
njia ya simu akiwa nchini huko ‘Ferguson’ katika mapumziko hayo ameweza kupata
mawazo ya kubuni rapu mpya ambazo zitaanza kutumika katika bndi yake hiyo.
Ferguson alisema amejipanga kuanza kuonesha rapu hizo wiki
hiyo kuanzia katika onesho lake la kwanza ambalo litafanyika katika ukumbi wa
SunSiro siku ya Alhamis.
Alisema kuwa katika ziara yake hiyo ya nchini Afrika Kusini
ilikuwa na mafanikio makubwa licha ya kuwepo ukweni.
"Nilikuwa nimeenda ukweni kwangu...lakini nimepata vitu
vipya ambavyo tutavifanya na wanamuziki
wenzangu wa Mashujaa na kuleta mabadiliko makubwa katika bendi yetu"alisema
Ferguson.
Ferguson, alisema kwa kutambua mchango wa wanamuziki wenzake
katika kuleta mabadiliko katika soko la muziki wa ndansi hapa nchini watakaa na
kuangalia wafanye nini zaidi ili bendi yao iweze kuja kivingine.
Hivi karibuni bendi hiyo ilipata wanamuziki wapya, ambao ni
Sudi Mohamed ‘MCD’, Charles Gabriel ‘Chalz baba’, Lilian Tungalaza Internet, na
Ally Akida kutoka bendi ya Twanga Pepeta.
Mashujaa Ijumaa itakuwa na onesho lake katika ukumbi wa
Business Park uliopo Kijonyama wakati Jumapili jioni itakuwa kwenye Bonanza la
kila wiki kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe.