TIMU ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imepata pigo jingine baada ya mshambuliaji wake Thomas Ulimwengu naye kuumia kifundo cha mguu.
Kuumia kwa Ulimwengu anayekipga katika klabu ya TP Mazembe ya Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kunafa timu hiyo kufikisha majeruhi wawili ambapo jana, kiungo wake Nurdin Bakari alichanika nyama za paja hali itakayomlazimu kukaa nje ya dimba kwa siku saba.
Daktari wa Stars, Mwanandi Mwankemwa ameiambia mamapipiro blog Ulimwengu alipata maumivu hayo wakati wa mazoezi ya timu hiyo kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam.
Alisema kutokana na maumivu hayo, Ulimwengu naye ataukjosa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Malawi utakaopigwa jumamosi kwenye dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
Stars inayonolewa na Mdenmark Kim Poulsen akisaidiwa na Mzalendo Sylvestre Marsh imepiga kambi kwenye hoteli ya Tansoma jijini Dar es Salaam ikijiandaa mechi yake ya mchujo kufuzu Kombe la Dunia hatua ya
makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast itakayopigwa Abidjan Juni 2 mwaka huu.