Makocha 35 wameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF) kushiriki semina ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) kwa ajili ya michuano ya vijana ya Copa Coca-Cola.
Semina hiyo itafanyika kwenye ofisi za TFF jijini Dar es
Salaam kuanzia Juni 4-9 mwaka huu chini ya mkufunzi kutoka FIFA, Ulric Mathiot.
Makocha hao wanatakiwa kuripoti Juni 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.
Makocha hao na mikoa yao kwenye mabano ni Englihard Livigha
(Mtwara), Joseph Sehaba (Dodoma), Ramadhan Ramadhan (Mjini Magharibi), Shaha
Khamis Rashid (Kaskazini Unguja), Salum Ali Haji (Kusini Unguja), Mohamed Ali
Khamis (Kaskazini Pemba), Mecky Maxime (Morogoro) na George Simon (Kagera).
Haruni Dudu (Iringa), Maka Mwalwisi (Mbeya), Amos Mewa
(Rukwa), Athuman Kilundumya (Tabora), Charles Mayaya (Shinyanga), Fulgence
Novatus (Mwanza), James George (Mara), Amani Kongoro (Kigoma), Mtoro Likere
(Ilala), Evarist Katomondo (Kinondoni), Shawal Bilanga (Temeke) na Rashid Chama
(Arusha).
Wengine ni Francis Samatta (Ruvuma), Issac Gamba
(Kilimanjaro), Aloyce Mayombo (Pwani), Jomo Puccey (Lindi), Justine Kanemela
(Singida), Charles Msengi (Manyara), Mohamed Kampira (Tanga), Alfred Itael
(Arusha), Nicholas Achimpota (Dodoma), Leonard Jima (Ruvuma), Leonard Malongo
(Mwanza), Kesi Abdallah (Tanga), John Memba (Ilala) na Zuhura Kapama (Kigoma).
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)