ALIYEKUWA Mhariri wa michezo wa gazeti la Mtanzania marehemu Rachel Mwiligwa anatarajiwa kuzikwa keshokutwa (jumatatu) nyumbani kwao Goba.
Marehemu aliyekutwa na umauti huo usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya Mwananyamala alipolazwa kwa ugonjwa wa Nimonia, awali ilipangwa azikwe katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Katika hatua nyingine, kampuni ya BigRight Promotion kupitia kwa mkurugenzi wake Ibrahim
Kamwe imepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mhariri wa Michezo
wa gazeti la Mtanzania, Rachel Mwiligwa kilichotokea leo (Mei 11 mwaka
huu).kwa niaba ya mabondia,makocha na mapromota wa masumbwi nchini
tunawataka familia ya rachel na kampuni ya New habari wawe wavumilivu
katika kipindi hiki kigumu cha msiba. Tunatoa POLE! - MUNGU AILAZE
ROHO YA MAREHEMU RACHEL PEPONI - "ameeein"
MAREHEMU RACHEL MWILIGWA KUZIKWA GOBA J'3, MASUMBWI NAO WAOMBOLEZA
byANID UPDATES
-
0